29 March, 2011

WHAT GOES AROUND COMES AROUND (UNAWEZAJE KUTUNZA UUAJI WA NAMNA HII?)

Daaah nilikua naperuzi blog mbali mbali pamoja na kusoma vitu vingi hiki kimenigusa na nina shangaa mtu unawezaje kufumbia macho ama kujishauri kuhusu mtu anaye ambukiza watu ukimwi kwa makusudi? ''What goes around comes around'' huwezi jua huyo dada anatembea na watu gani huko aliko usikute hata boyfriend wako ashampitia na kama bado iko siku.Chain ya ukimwi ni kubwa jamani tusipoteze muda kuokoa maisha ya wenzetu inapotokea kitu kama hiki.Mtu huwezi sema aah mbona mimi hainihusu huwezi jua huo UKIMWI  wa rafiki yako ukazunguka hadi kukufikia wewe.

Si jambo la busara kufumbia macho mtu yeyote anaye ambukiza watu virusi vya ukimwi tena kwa maksudi, kwa mtindo huu Tanzania bila ukimwi itawezekana kweli? Tena huyu msomi kabisa anadiriki kujiuliza mara mbili swala zito kama hili.Sasa ambaye hajasoma atafanya nini?

Kwa habari zaidi soma hapa:  http://beautytouchdar.blogspot.com/2010/07/rafiki-yangu-anaambukiza-watu-ukimwi.html#comments

''RAFIKI YANGU ANAAMBUKIZA WATU UKIMWI KWA MAKUSUDI, NIMFANYAJE? AU NIWAAMBIE UKWELI? ''


 Hicho ndio kichwa cha habari yenyewe mtu anaomba ushauri.(tafadhali fungua hiyo blog soma humo inasikitisha sana) Si kwamba ni unyanyapaa lakini kitu kama hiki sio cha kufumbia macho hata siku moja ni uuaji tena wa maksudi ambao hautakiwi kuukumbatia kwa namna yeyote ile.