Anyways tuache hio mimi binafsi ni Tomaso haswaa na nimejaribu kutumia mitandao mingi kwa kufuata masharti ya mtandao wa simu nikitaka kupiga simu bongo lakini ukweli ni kwamba matangazo tunayo ona ni tofauti na hali halisi mfano juzi juzi nimejiunga na mtandao mmoja hapa Uingereza matangazo yao ni kwamba ukipiga Tanzania ni pence 1 kwa dakika nimetumia pound 5 na simu imekata chini ya dakika 25!!!. Leo tarehe 11,July 2011 nimekutana na Tangazo la kampuni hio hio linasema kupiga simu Tanzania ni 10 pence kwa dakika nikafungua ukurasa wao kuhakiki ukweli nilichokuta sikuamini macho yangu DAKIKA 1 NI PENCE 19 NA SIO 10!!!.
Tangazo lao la leo
Kwa mujibu wa tangazo lao la kwanza kama kupiga simu Tanzania ni pence moja kwa dakika inamaana nilitakiwa kupata dakika 500 kwani Pound 5 ni sawa na pence 500 sasa nikawa najiuliza mbona imekata mapema? Nilichogundua ni kwamba dakika moja wanakata pence 20 na sio penny 1 kama tangazo linavyosema ..hio 20 ukiizidisha na dakika 25 unapata pence 500. Ina maana kama sasa imekua 10 pence kwa dakika basi ni dakika 50 kupiga Tanzania kwa Pound 5. Ila tangazo linakinzana na ukweli kwa maana ya viwango walivyopanga ukipiga simu Tanzania. kwa wale tunaopenda kupiga simu bongo kua makini na hii
Ukienda kwenye mtandao wao kuona bei halisi unakuta habari tofauti angalia mwenyewe hapo chini
PAYG Rates
International PAYG Rates
Select your destination to check the rates.
Destination | |
Rates | |
---|---|
Landlines | 5 pence per minute |
Mobiles | 19 pence per minute |
SMS | 10 pence |