13 May, 2010

Burudani anga za bongo flava..

Watu walisema sana kama huu muziki wa kizazi kipya hatutafika popote/mbali kutokana na watu kuingia kwa fujo/kasi lakini siku hadi siku wazidi kufanya vizuri na hatimaye kupiga hatua japo sio kwa wote. Ni vizuri kuona vijana walio wengi wanapata kujiajiri kupitia nyanja hii japo sio wote wameweza kutoka kimuziki.Si vibaya kuwapa moyo ili waweze fanya vizuri zaidi.Ukiachia mbali burudani muziki unaweza kuelmisha kwa kufikisha ujumbe mbalimbali kwa jamii.Kwa maana hio basi tunategemea kuona wahusika wakiwa wamejipanga kutoa burudani, elimu n.k

Nimependa collabo hii ya Albino fulani, Sugu, mwana FA, na Belle9 katika wimbo NAFASI.Mistari yote iko poa kwa mtazamo wangu ila nimeguswa na mistari ya FA eti ''wafungwa wangetembelewa na mademu na wake zao'' hili nalo ni neno hivi wale jamaa kule jela SEGEREA na kwingineko wanaishi vipi ukizingatia kama binadamu wanapata hamu ya kufanya mapenzi! Mbaya zaidi wengine wameacha wake zao wapendwa na wa ndoa kabisa huko majumbani.Kuna habari zisizo rasmi kugeuzana huko jela je wimbi la mashoga litaisha kweli kwa mtindo huu?? sasa hivi ukiingia chatrooms za kiswahili hukosi shoga ni wengi hadi kero lol..japo hata chatrooms za kiingereza wapo inashangaza kwa Tanzania nchi changa kabisa kua na kiasi kikubwa cha mashoga....hali kadhalika wale wa kusagana nao wazidi ongezeka sijui tunaelekea wapi?!..well turudi kwenye track/muziki huu wa kizazi kipya.

Wanasema penye nia pana njia pamoja na kwamba vijana wengi wanapenda kuingia katika muziki bahati mbaya wachache ndio wana ng'ara siku hadi siku wakati wengine ndio wanapotea.Lakini ni mambo ya kujipanga tu wazuri katika fani hii wata ng'ara na wale wasiojipanga watapotea KIMYA KIMYA...Hivi yule Mr Nice na takeu style yuwapi? Alitamba na vibao ''FAGILIA,KIDALI POA,YEBO YEBO na nyingine nyingi. Wapi Hard blasters? Uswahilini matola waliwahi tamba na kibao 'KOSA LA MAREHEMU', wapi Mwana wa komba (Caz-T)- aliwahi tamba na kibao ''NAKUHITAJI'' n.k aaah nimesahau wengine wengi nikikumbuka nitawataja au kama vipi nitajie lol.




Ujumbe huhusu simu za mkononi hahahah hawa jamaa nyimbo zao hua sina mbavu, wasikie mwenyewe mimi sina la kuongeza zaidi ya kusema tu kua makini na simu yako maana wewe ndo waijua namna unavyoitumia na namna inavyokusaidia kwa ishu zako za kila siku.

No comments: