Nachukua fursa hii kukusalimuni nyote wanaukumbi.
Hapa,Zanzibarwebsite ni pahala panapowaunganisha wazungumzaji Kiswahili popote walipo duniani.
Hilo ndio lengo mama.
Mengine kwa kupitia lugha yetu hii unapata haya yafuatayo:
- Kujifunza taaluma mbali mbali kupitia kwa wenzako waliokuzidi.
- Kujipatia taarifa mpya na zilizopita
- Kujipatia Rafiki /Shoga
- Kukutanisha na wenzako ambao mlipoteana kwa masiku.
- Kujiliwaza kwa picha/habari/mazungumzo/muziki n.k
- Kutumia uhuru wako wa kusema ( freedom speech) na kusikilizwa.
Hili la 6 - Ndio la kuwa makini - UHURU WAKO isiwe ukajisahau kutoheshimu UHURU WA WENGINE.
Ili kulinda mipaka ya uhuru wa wengine na wako mwenyewe ilipaswa haya yafuatayo uzingatie:
- Heshima na Nidhamu- usiropoke matusi makavu makavu.
- Usilete mas-hara ya kuchupa mipaka ya kumuingia mtu maungoni - kiasi cha mtu kujiona amedhalilishwa ama kudharauliwa.
- Epukana na Ubaguzi wa aina yeyote iwe rangi/jinsia/kabila au wakimajimbo.
- Uwe tayari kutoa mchango ili na wewe uchangiwe mawazo.
- Uwe tayari kukosolewa pale unapokosea.
HAYA YAKIZINGATIWA NA KUFANYIWA KAZI - Zanzibarwebsite will be the place of leisure,educative,harmony and more communicative one rather than others.
Shime wadau- HESHIMA NI KITU CHA BURE
Babengwa wa Upendo.
Zaidi watembelee Zanzibarwebsite