25 July, 2011

MADUKA YA BIDHAA FAKE ZA APPLE YAFUNGWA

Nilikua nashangaa pamoja na vitu vya Apple kuwa gharama lakini speed ya utumiaji imekua kubwa kutokana bei kua rahisi kwa baadhi ya vitu kumbe kuna Wachina walikua waki supply fake apple products kimya kimya huko Kunming city ambako serikali ya China imewashitukia na kufunga hayo maduka mara moja.


Sasa najiuliza hivi sisi tunashindwaje kuwa na serikali kama ya Wachina?  Bidhaa fake kila mahala na mbaya zaidi zote ni imported  na TBS tunayo!!!! Hapo hatujajua viwango vya bidhaa ambazo ni made in Tanzania!.Yaani nawaza tu kwa sauti bila kupata majibu wachina waliopo bongo wanauza tv na vitu vingine fake watafungiwa lini maduka yao? Sasa hivi ukinunua hata simu Guarantee unaambiwa ni 2 weeks!!. Wenzetu mfano hapa UK simu ina Guarantee kuanzia  mwaka mmoja na vitu vingine miaka 3 na  kuendelea na ni Made in China.Sasa inakuwaje Bongo iwe 2 weeks?

Kwa habari zaidi ingia HUMU