18 May, 2010

Matumizi ya simu kwa madereva barabarani

Imekua ni kawaida sana kuona mtu anaendesha gari, pikipiki,ama hata baiskeli huku akiandika meseji kwneye simu yake. Tukichukulia ule usafiri wa umma kama bus na usfairi miwingine kama taxi au Coach, school bus na zingine.Ivi nini wajibu wetu kama abiria unapokua kwenye bus au taxi na kuoana dereva yuko busy na simu huku anaendesha? Busy nina maana kutuma meseji au kuhangaika kupokea simu wakati gari liko kwenye mwendo mkali. Ukiacha yeye mwenyewe kua hatarini kuacha njia anaweza pia sababisha ajali kwa madereva wengine.

Wataalamu wa mambo ya usalama barabarani Virginia Marekani, wamesema kuna asilimia kubwa kwa dereva anaye endesha gari huku akitumia simu ya mkono kupata ajali, au kusababisha ajali kwa madereva wengine wanaotumia barabara wakati huo.Wataalamu hao kutoka chuo cha usafiri cha Virginia, wanasema kugonga au kugongana na gari jingine kuanaweza kutokea wakati wowote wakati dereva anaandika meseji ama kupiga na kupokea simu ya mkono huku akiwa anaendesha gari.



(video za ajali zinazo sababishwa na na matumizi ya simu gari likiwa ktk mwendo).




(dada anayetumia simu wakati anaendesha)

Hizi ziko sana bongo hapo akikugonga anasema samahani bro au sis…mie simuelewi mtu kwa hili !!

Wataalamu hao wanazidi kudai hakuna sheria kamili inayotaja kosa la kutumia simu wakati unaendesha bali ipo tu ya makosa ya jumla mfano: kuendesha gari kwa uzembe barabarani (reckless driving). Ambayo inamtaja mkosaji kua nakosa ya kutojalia usalama wa wengine, mali, hata kuhatarisha maisha.Hivi sasa majimbo kama California, Connecticut, DC, new Jersey, new York, Oregon na Washington wamezuia matumizi ya simu kwa madereva wote sio tu waendesha mabasi na madereva walio chini ya miaka 20 kama ilivyo kua hapo mwanzo.

Hata hivyo kukua kwa teknolojia ya simu kumechangia kwa kiasi kuongezeka kwa ajali za barabarani kutokana na kwamba watu wamekua wakitumia simu wakati wanaendesha. Kwa maana hio kuna haja ya kuanzisha sheria inayo husu matumizi ya simu kwa madereva ili kupunguza ajali za barabarani. Chini hapa ni baadhi ya video zinazo onyesha ajali mbalimbali kutokana matumizi ya simu wakati unaendesha barabarani.