19 May, 2010

Money is not a problem, the problem is how to use it!

Muziki unapotumika kutoa ujumbe ambao kila mtu aweza kua na mtazamo tofauti.Huyu anasema money is not a problem, problem how to use it..je ni kweli? unaweza jiuliza unavyotumia pesa zako kama ni sahihi ndo zinavyotakiwa kutumika? Hapa najua kila mtu atakua na jibu lake kutokana na kuwepo mitazamo tofauti.Hata hivyo usawa wa matumizi ya pesa kwa kila mtu ni vigumu kuutaja kwani kila mmoja anaona halali kulingana na matakwa yake yanavyo weza kutimia vile atakavyo.

Tuwekee mfano yule mwanamme/mwanamke anayetumia pesa zake kuhonga mwanamke/mwanaume na kufanya nae mapenzi tena BILA KINGA kwa kiburi cha pesa zake na kwa makusudi kabisa kumwambukiza ugonjwa (UKIMWI) mtu mwingine, je ametumia pesa zake sawa? hapa jibi litakua HAPANA! JE anaye honga wanafunzi na kuwapa MIMBA? (hapa ni vijana na mijibaba) Vipi kuhusu Mijimama (samahani) inabidi tu niseme! inayo honga vijana wadogo aka serengeti boys na kufanya nayo hayo wanayo yafanya? .tena wengine wakishapata hio mishahara walio sotea kwa sana kinachofuata ni kulala BAR.Nadhani wale wanaoijua Bia moja Tz aina ya Bingwa wakati inaingia watu wengi walilazwa hadi mahospitali maana ile ukinywa kama safari utajua maana ya pombe nini.Sijui bado ipo! na kama ipo ni wazi watu wanaiogopa maana wengi iliwafanya mbaya hasa walimu.

Ntombi (ni jina la mwanamziki sio tusi kama unavyotaka kufikiri lol!) anasema Money is not a problem , the problem is how you use it..je wewe unasemaje kama ukiulizwa?
sambamba na hio angalia video hii watu walivyo changamka na usiite walevi utapigwa bure ita walipa kodi wazuri aka wanywaji!!Sina mengi sana kwa leo ila tu jiulize kama matumizi yako ya pesa ni sahihi ama sio sahihi.Tena wengine bila aibu unakuta anatumia hata kuzidi bajeti aliyo nayo.Kama ni mfanya kazi ataacha kua mla rushwa kweli mtu wa namna?? Na kama ni mfanya biashara je ataacha kufanya biashara Haramu?.Kama matumizi yanazidi kipato wapi atafidia kama sio njia za panya/zisizo halali?.

Pamoja na yote haya bado nchi kama Tanzania imeendelea kua na tatizo la mishahara midogo kwa wafanyakazi kitu ambacho kina karibisha rushwa kwa kishindo kabisa.Kwani hawa wafanyakazi kama kima cha chini kwa mujibu wa TUCTA kua 315,000/= basi ni wazi rushwa haitaisha. Kwani mnfanya kazi huyu huyu ana majukumu yanayozidi mshahara je pesa atatoa wapi?.Kwa kweli nimecheka kuona hii katuni lakini ina ukweli ndani yake, na si kwamba nimecheka nafurahia ila kuna baadhi ya vitu vina chekesha kama NYUMBA NDOGO ( sio lazima kua na nyumba ndogo kwanini uwe nayo? inachekesha sana kwa kweli mie naita mtu mzima ovyo hata kama ni private life ya mtu!)

Hongera kwa mchora katuni, ebu angalia mwenyewe hio katuni halafu sema kama 80,000/= inatosha chochote. Hata ada tu haitoshi,bill ya umeme? maji? kodi ya nyumba?.yani huyu ndio apewe ofisi aache kufungua bucha?.Sina maana walipwe vizuri ili kumudu nyumba ndogo bali mahitaji ya msingi kama baadhi ya ambayo yameonyeshwa kwenye katuni.ok hata tuseme huyu mtu hana mke still hii pesa haitoshi sasa ana mudu vipi maisha? Hii ni sawa na useme mlinzi analinda bank kwenye mamilioni ya pesa halafu mshahara duni je wezi wakija wakala dili naye nani atalaumiwa? kuna vitu vingine zinatia vishawishi mtu analinda mamilioni halafu analipwa kiduchu yani hio ni sawa na simba kumpa alinde nyumbu!!
Kwahio hapa nimedokeza mambo mawili kwa pamoja ambayo yatafanya ujiulize ni yapi ndio matumizi halali ya pesa tulizo nazo hio mosi, pili,je mishahara tunayo lipa wafanya kazi wetu inakidhi mahitaji ya msingi tukiondoa yale yasio ya lazima?

No comments: