11 March, 2011

JAPAN YAKUMBWA NA TSUNAMI

Japan imekumbwa na tetemeko kubwa la bahari maarufu kama Tsunami ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa mali na maisha ya binadamu mapema leo.Tetemeko hilo  kubwa kiasi cha 8.9 magnitude limeripotiwa kuathiri sehemu kubwa ya maeneo ya pwani kaskazini mashariki mwa Japan ambako mamia ya watu wana hofiwa kufa kwa kuangukiwa na nyumba na mafuriko makubwa ya maji yaliyo tapakaa toka baharini na kubomoa nyumba,kuzamisha magari,meli na kusababisha moto mkubwa baadhi ya maeneo.

Tetemeko hilo  la kihistoria limepelekea kuzimwa kwa mitambo minne ya Nuclear ambayo hutumika kufua umeme wa Gigawatts 11.Halihiyo imepelekea maeneo mengi kuwa bila umeme.Japan  ni moja kati ya nchi zinazo zalisha umeme kutumia Nuclear na asilimia 30 ya umeme wake hutokana na nishati hio.


                            (Ramani ya Japan)


Wataalam wa mitambo hio wame tahadharisha kuhamisha watu wote karibu na mitambo hio iliopo pwani ya Japan maeneo ya Fukushima na Fukui kwani tetemeko limeathiri mitambo hio na kuweza kupelekea uwepo wa mionzi inayo athiri watu au hata kusababisha vifo.Kudhibiti hilo marekani imeripotiwa kupeleka kipozeo cha mitambo hio baada ya kilichokuwepo kuharibiwa kutokana na tetemeko hilo.

Kwa picha zaidi na Video toka BBC  bonyeza kwenye link :http://www.bbc.co.uk/news/world-asia-pacific-12709847. Pia videoa toka RT angalia chini

                                                                 RT (2 mins Video footage  11/03/2011)