19 May, 2010

Utani wa kijinga!!!

Radio Dj mmoja wa shirika la utangazaji BBC kituo cha jijini Birmingham jumatatu ya tarehe 17 mchana aliropoka na kusema Malikia kafariki dunia.Kama haitoshi inadaiwa kua Dj huyo alipiga wimbo wa taifa kusindikiza tangazo lake.Mtangazaji huyo kwa jina Danny Kelly, 39 amekiri kukosea tangazo na kuomba radhi kwani alikua na tangazo tofauti na maalumu kwa wasikilizaji wake ambalo lilimfanya amtaje Malikia bila kukusudia.

Habari zaidi zinasema Dj huyo amekiri kukosea tangazo muda mfupi baada ya kutangaza na hatimaye kuomba radhi kwa wasikilizaji na kwa mhusika mwenyewe.Baadae shirika kubwa kabisa la utangazaji hapa Uingereza liliomba radhi pia kwa kosa hilo ambalo limechukuliwa kama ni utani alio ufanya mtangazaji huyo dhidi ya Malikia.

Hata hivyo inadaiwa mtangazaji huyo ni mahiri kwa kuchekesha wasikilizaji wake kwa kufanya utani mwingi katika vipindi vyake au status message ambazo amekua akiandika kwenye mtandao wa kijamii maarufu kama facebook.Vyombo vya habari vimesema BBC imemsimamisha kazi kwa muda wa wiki moja na pengine hatua zaidi zikachukuliwa dhidi yake kwa kosa alilofanya.

No comments: