24 May, 2011

UFUNGUKAJI WA WASANII WETU OVYO!!

Hapa chini ni video ya Clouds Tv 'Take one' 'MTU KATI' na Zamaradi.Angalia vizuri hii Video clip then sikiliza mtu kama msanii ambaye ni kioo cha jamii anapo ongea katika chombo cha habari.Kuna kipengele anasema usanii wake umemuweka karibu na mabinti,imempa mademu,imemuongezea upendo kwa mademu!!! huyu ndio kioo cha jamii!! ...Ninge elewa angesema usanii wake umemuweka karibu na watu SIO MADEMU (HII NI PUMBA).Pia anasema hua anafanya ukauzu kwa mademu wanao mtega kwa kuvaa miwani tinted kwa maana hio ''katufanyia ukauzu Watanzania tunao angalia hii interview kwa kutuvalia hio miwani'' MAELEZO YAKE HAYAJA JITOSHELEZA!!

Si kwamba na 'hate' kwanza simfahamu namsikia tu....Kiukweli ameongea kituko cha mwaka coz movie hawangalii mademu peke yao,aidha kwenye hii interview MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI.. nimependa kipengele cha matumizi mabaya ya lugha katika movie zetu (movie editors kama wapo wawe makini na kazi yao) na sehemu nyingine zote uozo mtupu na ameaibisha wasanii wenzie (mtazamo wangu)...sikiliza halafu nipe mtazamo wako pia (ni mtazamo tu)

Msikilize Hemed akifunguka hapa chini (Aibu)
(kwa hisani ya Zamaradi Mketema)
                                                         

Vituko vingine vya wasanii angalia hapa: http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/hasheem-thabeet-afanya

No comments: