24 May, 2011

FACEBOOK KIBONGO BONGO..

Mimi nimejiunga facebook ili kukutana na marafiki niliopotezana nao muda mrefu mfano Classmates,School mates, University mates,Work/field mates na wengine ili kujuliana hali (kuwasilina kama marafiki), kudumisha  urafiki na kupashana habari zinazo tokea kila mtu alipo kwa wakati ule.Facebook inasaidia kupata marafiki mlipotezana nao hata marafiki wapya na kuwakutanisha

                                                           Facebook logo

Facebook inasaidia kukutanisha watu kwa matukio mbalimbali ya kijamii mfano weddings,parties,kucheza games mbalimbali,kutangaza biashara; kisiasa mfano: mikutano,maandamano; kisayansi mfano: kuendesha mijadala ya kitaaluma na mambo ya teknolojia i.e IT,.Huko Egypt (Misri) Facebook imesaidia kukutanisha watu ambao wameweza hata kuing'oa serikali ya  muda mrefu ya Hosni Mubarak  (14 October 1981 – 11 February 2011) na hata watoto kubatizwa 'Facebook' kama kumbukumbu ya tukio hilo.

Watanzania wengi tumejiunga Facebook kwa kasi kubwa tu,ni vizuri japo sijajua kama matumizi ya huu mtandao yapo sawa! Kwa mtumiaji wa facebook unaweza kua unanielewa.Wengine picha tunazoweka humo ni utata mtupu mfano mtu kaweka picha ya makalio yake tu yakiwa tupu ama nguo inayo onyesha maungo,shanga kiunoni,lips peke yake,au mwili wote ukiwa  na chupi tu,kifua wazi ili iweje? au mtu kaweka picha yenye maneno 'I've the p**sy (ni tusi siwezi andika lote)  so I make the rules' ili iweje?.

Tujiulize tumejiunga facebook ili iweje?.Mtu unakuta yupo ofisini the whole day yuko online (sio idle)  facebook hio kazi anafanya saa ngapi? Mimi nimeona facebook kwa bongo ni 'more of a dating site' je wewe unaionaje? au unaichukuliaje?.Kiufupi madhara ya facebook ni makubwa kuliko, mfano watu wengi wamefukuzwa kazi,ndoa nyingi zimevunjika,watu wengi wameuawa kwa kupitia facebook hasa wale wasio ogopa kukutana mtu usiye mjua,kubakwa,kufungwa, mahusiano mengi yamevunjwa,na watu wengi  sasahivi hufuta (deactivate) akaunti facebook wanapooa,kuolewa ama kugonganisha wapenzi.Be careful na facebook kabla huja umbuka...na pia nijibu......

                                        Wewe umejiunga facebook ili iweje?
                                      Kiraka amejiunga facebook ili......

                                     Ochu anajibu hilo swali msikilize hapa chini




4 comments:

Mwanasosholojia said...

Mkuu ni umenena kitu cha msingi sana hapa!Hata mimi pia ni "memba" wa Fb kwa sababu takribani sawa kabisa na ulizoziainisha. Hapa nafikiri ni suala la rationality na uhalisia zaidi. Matumizi ya social networking kama Fb yanakutegemea wewe mwanachama zaidi, ni kujipangia,uitumiaje, muda gani, kwa manufaa gani na kwa akina nani (ndiyo maana kuna category ya kuchagua unachopost, akione nani na nani asikione)

Hapo ndipo tatizo linapokuja nafikiri, wengi wetu hatufahamu hilo na nadiriki kusema tumekuwa careless, tuna-post tu bila kuangalia. Kuna suala la security na privacy hapa, wabongo wengi hatulijali kabisa! Kwa sasa ni rahisi sana kwa mtu kuweza kukufuatilia na kupata taarifa zako za muhimu, na hata kukudhuru au kukuhujumu kama ulivyosema,kupitia hizi social networking!

Sina haja ya kurudia madhara uliyoyaainisha mkuu kwa kuwa yameshaonekana na yanazidi kuonekana, lakini labda kujaribu kuchangia nini kifanyike. Elimu juu ya matumizi ya hii mitandao inapaswa kuanza kutolewa. Wenzetu Ulaya wanafanya sana research sasa hivi kuainisha mambo ya security na privacy katika mitandao jamii. Wanatoa ripoti na zinapatikana. Tutumie ripoti hizi kujalibu kuelimishana kwenye baadhi ya mambo.

Pia, ingawa ni ngumu kidogo, suala hili inabidi lianzie kwa mtu mmoja mmoja (mtu binafsi). Jiangalie mwenyewe, thamini muda wako (hukatazwi kuingia na kupost chochote) angalia tu unatumia muda kiasi gani na unachofanya kina mantiki gani. Sambaza role hiyo mpaka kwa wengine. Kwa sasa si ajabu hata watoto wa shule za msingi wana kurasa zao za Fb! Hatukatazi, ni teknolojia ina pande mbili, lakini sisi tuwe chachu basi kwao kuwaelekeza nini cha kufanya. Tukumbuke, moja ya taasisi za socialization ya watoto ni familia. Sisi tuna mchango gani katika familia zetu juu ya hili?

Nashukuru mkuu, kwa sasa ni hayo tu.

Rik Kilasi said...

Mkuu Mwanasosholojia kwanza niseme pamoja sana kiongozi...hii facebook kwakweli tutakuja kujuta kuifahamu kama hatutakua makini hebu mimi nawewe tuanze na wale watu tunao wajua kutoa hio elimu kabla haijawa too late!.

Mie sasa naifananisha fb na simu ya mkononi ambayo ime rahisisha kabisa watu kukutana hasa ukiwa na no ya simu,kutongozana ndio usiseme,kudanganyana ndio kwa sana mtu anasema yuko nyumbani/ofisini wakati yuko Bar au Guest kabisa..sasa Fb imekua rahisi zaidi maana unaona na picha ya mtu hata kama humjui unaweza mtumia msg ,wengine kama hakujui ana ku 'poke' kwanza ukijibu unaye!! hahaha..sasa shida inakuja ukigonganisha magari ndio hapo option ya ku deactivate account inapo tumika (wengi sasahv huitumia sana)..mie mpaka sasa sijui idadi kamili ya marafiki zangu fb coz leo unakuta 150,kesho 145,keshokutwa 148 Confusing!!!

Watu wengi ukiangalia profile zao security & privacy setting hakuna unaweza ona unachotaka na unaweza comment hata kama sio rafiki yako..hizo setting za nani aone ulicho post facebook sijui hawajui au ndio bora mtu upo facebook! maana FB imekua kama fashion sasahv..sasa humo ndio unakuta mtu ka post pic kifua wazi hasa wanaume, wanawake hawapo nyuma nao nyonyo waziwazi na mikogo mbali mbali picha za khanga tupu,nguo za kulalia,au nguo inayoonyesha maungo kama yalivyo 'sijui ndio biashara matangazo?'

Wengine pia hudiriki kuweka picha za watoto ama watu wengine sijui nao wana maana gani?.Hata kama Fb unaamua uitumieje wengine matumizi yake sio kabisa mpaka kero.

Najua wanao tongoza/tongozwa ni wengi ila wapo wanao jitakia..mfano kama hutaki kutongozwa kwanini uweke picha za mitego? ili iweje?.

Mimi nashauri kama una mdogo wako yuko under 15 ni vema akaachana na fb kwa sasa ajiunge akiwa matured,fb vijana walio katika age kama hii ndio wana add kila mtu bora kaona picha nzuri,watu kama hawa kudanganyika ni rahisi kwa maana hio maisha yao yako hatarini..na wale tunao ombwa kufungua akaunti za fb watu wengine ni vzuri kuzingatia umri wake, na tulio tayari watu wazima tuwe makini na facebook kama sivyo tutaumbuka.Kama mtakua na kumbukumbu enzi za Zeutamu watu wengi walilalamika kuibiwa picha fb (sasa tulio weka fb kama album, tuangalie na picha tunazoweka na nani azione)si kila picha ya kuweka fb,pia si kila kitu cha kuongea fb!!, majina ya facebook nayo vituko unakuta mtu kaandika Juicy...sweetlips....,hotbabe..,mb** kubwa....,lovesex apple..duh, well kama nilivyo sema awali ni mtazamo tu, ngoja tusikie wengine mitazamo yao.

Anonymous said...

Ni mara yangu ya kwanza kutembelea hii blog na niseme kuwa ina mambo mazuri ya kuelimisha,hongera. Kuhusu FB ni kweli inakutanisha na watu ambao tumnepotezana nao siku nyingi. Ila WaTz tunaitumia vibaya urtakuta mtu anapiga pics ambazo ni nusu uchi na kuziweka FB. Na wengine ni wake za watu lakini bado pics anazoweka hapo ni za ajabu. Na akitongozwa anakasirika na kuanza kutukana...ila ungejiheshimu hakuna ambaye angekufata. Na pia ugomvi na vijembe visivyo na maana. Watu wanatukanana na kukasirikiana, Nakumbuka mmjoa wa rafiki zangu alikasirika kwasababu sikutoa maoni kuhusu birthday yake. Mtu anakupangia cha kufanya eti wewe ni rafiki gani ambae hata hutoi maoni ktk pics zangu. Kama mlivyosema wengine wanatoa sifa ambazo hata haziendani. Aidha ni ulimbukeni au ni ujinga uliokithiri waTz.

Rik Kilasi said...

Anon wa saa 14:38 nashukuru sana kwa compliment, pia kutembelea blog hii.Katika watu ambao wanaona ukweli wa kilicho ongelewa hapa wewe unaweza kua mfano mzuri kwani umeonakabisa.Sasa mtu anapokulazimisha uweke comment kwenye picha zake anataka nini? after all sio lazima!

Mie nishaona picha moja mbili tatu za utata kabisa humo FB na kwakua profile zake hazina privacy nikafungua ndio nilipoona status ya ''In a relationship & Married sasa nikawa najiuliza kama yupo kwenye mahusiano na picha ya mitego kaweka yann na pale pa kujieleza katoa onyo kali'' sitaki meseji za mapenzi/kutongozana ama kuuliza mambo mengine unachoona hapa FB ndicho unacho takiwa kujua'' mwisho wa kununukuu...hio picha ukiona huwezi acha kutongoza!!

Watanzania kwa ujumla (sio wote) wanatakiwa kua makini na matumizi ya internet unakuta mtu yuko facebook,yahoo messenger,msn,skype,au chatroom hakuna cha maana zaidi ya kutongoza na kutegana.Sikatai njia muafaka kwa anayetaka kufanya hivyo lkn isiwe ndio kila siku kazi ni hiyo ,tusiende mbali wenzetu wakenya ukimkuta chatroom kama ana biashara basi hilo ndilo la kwanza mengine hufuata..wakati huo huo wabongo tutataka kufahamiana jinsia kuangalia uwezekano wakuchakachua nakadhalika.

Ni imani yangu wachache ambao wanajua kwanini wako facebook wata waelimisha/kuwakumbusha wale wasio makini na mwisho wa siku hapo baadae pengine mambo yatakua sawa.