24 May, 2011

LIMO YA OBAMA MAARUFU KAMA ''BEAST'' YABUMA ZIARANI IRELAND

Gari moja wapo katika msafara wa Obama  huko Ireland yabuma baada ya kugonga tuta nje ya ubalozi wa Marekani jijini Dublin-Ireland.Gari hilo aina ya Cadillac la Mr Obama lenye jina maarufu kama ''The Beast'' Yaani 'Mnyama' kwa kimakonde lilisekana kubeba wataalamu wa ulinzi katika msafara huo wakati Rais wa Marekani Barack Obama akiwa ziarani nchini humo jana tarehe 23/05/2011.

Umati mkubwa wa watu umeshuhudia tukio hilo 'live' ambapo mlio mkubwa ulitokea baada ya chesis lake kugusa tuta na kushindwa kwenda mbele na muda si mrefu waliletewa gari lingine kuendelea na msafara.


Kama uonavyo kwenye video hapo juu hicho ndicho kilichotokea.Limo/The Beast hilo lina  urefu wa futi 18 na uzito wa tani 8 na upana wa chuma cha bodi wa inch 8 halipitishi bomu wala risasi na lina lina oxygen yake ndani.Rais Obama akiwa ndani ya hilo gari nick name yake inakua Cadillac one na sio The Beast.  The beast inasemekana kua na camera kila kona,shotguns na vingine vingi kwa ulinzi zaidi                               


Mafundi wakinasua The Beast iliponasaThe Beast katika mchoro

(chanzo:dailymail)

                                                                                                                                                                            

No comments: