24 May, 2011

SIMBA SC KUVAANA NA BIRMINGHAM CITY FC JULY 7 MWAKA HUU

Timu ya mpira Simba Sports Club ya Dar es salaam kuvaana na Birmingham City Football Club ya Uingereza Julai 7,2011.Hayo yatategemea kuthibitishwa baada ya timu ya wataalamu toka Uingereza kuona kiwango cha uwanja na mazingira kiujumla kimichezo baada ya kukagua tarehe 16/05/2011.Kama mechi hio itaridhiwa Birmingham City ita ambatana na mashabiki  wasio pungua 1000 watakao jilipia gharama za safari na malazi wenyewe wakati timu itajipatia vijisenti visivyo pungua Dola Million 1.2 na kulala hotel nzuri.

                                kikosi cha timu ya simba

Mpaka sasa safari ya BCFC kwenda Tanzania haijathibitishwa baada ya ukaguzi ulio pangwa ufanywe tarehe tajwa hapo juu na pia kutokana na ratiba za mechi za hapa ulaya.Baada ya hayo yote kukamilika ndipo safari itathibitishwa.Pia nimetembelea mtandao wa Simba SC (http://simbasportsclub.co.tz/v3/)  hakuna taarifa yoyote kuhusu mechi hio sasa sijajua mashabaki tutajua nini kinaendelea maana menu zenyewe hazina maelezo yoyote yaani hata menu iko empty: Mfano events,matches,News hakuna kitu-sijui labda nimeingia sio site yenyewe kuna anayejua anipe site halisi please! maana kama ndio yenyewe bado hatupo siriazi kiukweli maana haina cha maana zaidi ya orodha ya viongozi,wachezaji na historia ya timu!!!!!.Angalieni Yanga http://www.yangasc.com/

Anyways, hongereni Simba kama hio mechi itachezwa na nawatakieni ushindi dhidi ya wazungu!.

soma zaidi hapa:http://www.goal.com/en/news/89/africa/2011/05/03/2469421/birmingham-city-officials-to-inspect-facilities-in-tanzania
                          : http://www.birminghampost.net/midlands-birmingham-sport/west-midlands-sports/birmingham-city-fc/2011/04/18/birmingham-city-tanzania-confirmed-as-potential-destination-for-pre-season-tour-97319-28542251/

No comments: