01 May, 2011

TOKA ZE COMEDY ORIGINO MPAKA KUHUBIRI NENO LA MUNGU!!!

Video  ya kwanza hapa chini inaonyesha 'Masanja Mkandamizaji' anakandamiza nini mimi sijui!! au jina halisi Emmanuel Mgaya akihubiri neno na kudai yeye kaokoka na wajanja wote wameokoka (ni kweli wajanja wote wameokoka mie sijui, wajanja ni akina nani pia sijui!,yule aliyekua pembeni yake wakati akihubiri pia simjui).Ila niseme tu ni mwanzo mzuri kwa wasanii kuokoka kwani wana nafasi ya juu kabisa ya kurubuniwa na shetani kutokana na kujulikana kwao kwa jamii hii itawasaidia kama kweli wana maanisha KUOKOKA ISIWE MWAVULI WA KUFICHIA MAOVU na NI LAZIMA WAO KAMA KIOO CHA JAMII WAWE MIFANO YA KWELI NA SI VINGINEVYO !!. (ni mtazamo tu)

Baada ya kusema hayo ningependa jamii yetu ya Kitanzania kujua maana halisi ya 'KUOKOKA'.kwa kusoma na kuelewa maandiko sio tu kuamini kila tunacho ambiwa ndio ipo siku tuje kuchomana moto eti mwisho wa dunia eti Mungu kasema!! Mfano Kibwetere wa Uganda alichoma moto kanisa ndani kukiwa na waumini!! kwakua watu waliamini kila alichosema hata waka kubali kuchomwa moto.Tusiwe wavivu wakusoma vitabu vya maandiko matakatifu.

.Mimi inapofika hatua ya kuongelea imani zetu huwa sina ubishi kwakua naamini kila mtu ana imani yake na Imani ya mtu ndio inatakayo muokoa.Kama mtu hana imani ni kazi bure kusema ameokoka,vivyo hivyo kama mtu una sali kanisa fulani ambalo unadhani ukiwa huko ndio umeokoka  bila ya Imani hapo mtu unakua unapoteza muda wake bure.Au mtu kutumia kanisa fulani kama mwavuli wa kuficha maovu wakati ukweli ni kwamba umeoza!! Utakuja kuwa kuni za kuchomea wenzio huko eternal hell (kuzimu)Nijuavyo mimi kama nilielewa vizuri mafundisho ya dini...Imani ya mtu huanza na kuamini  uwepo wa Mungu na kukili imani yako kwa kinywa chako.Ni lazima uamini Mungu katika NENO LAKE (maandiko matakatifu) pia umtumikie ndipo udai wokovu wake kwa imani uliyokua nayo. ...na hapo ndipo nguvu ya Mungu itakuokoa, itakulinda, na kukuwezesha kuishi maisha mema katika yeye muweza wa yote.Ni lazima tutambue imani ya mtu haichezewi na ni vema na haki kuiheshimu.KUOKOKA KUNA MAANA KUBWA ZAIDI YA KUONGEA.....HATA HIVYO SINA MAANA WANAO SEMA WAMEOKOKA WANA TUDANGANYA ILA KAMA WANAONGEA WAKATI MOYONI WANAJUA SIO BASI WANAJIDANGANYA WENYEWE.WALIO OKOKA KWELI MUNGU AWAJALIE.

The Bible says: 'Our hearts are deceitful, we should not trust in our hearts (Jeremiah 17:9)
                          'There are false christs,false gospels,and false spirits ( I Corinthians 11:4)
                          
So how can you be sure that you've heard of the true Gospel,received true christ and the true Holy Spirit??! Comrades we must be certain that our faith is THE TRUE FAITH IF AND ONLY IF BASED ON SCRIPTURE AND NOT THEM FALSE ONES BASED ON FEELINGS!!!

Angalia hizi Video hapa chini zinafundisha zaidi maana ya kuokoka2 comments:

U.S.A said...

masanja your the best we love u!!!!!!!!!!!!from u.s

U.S.A said...

MASANJA YOUR THE BEST..KEEP IN TOUCH WITH JESUS..LOVE FROM U.S FANS