29 April, 2011

LEO MAMBO YOTE ROYAL,KAZI TUTAFANYA AKISHAOA!!

                                                                      Kate & William

Ni ile siku iliyokua ikisubiriwa kwa hamu ambayo mjukuu wa Malikia Elizabeth wa pili Prince William anamuoa mchumba wake wa siku nyingi Kate Middleton.Ni siku ya kihistoria zaidi ambapo maandalizi ya harusi hii ya  familia ya malikia yamechukua muda mrefu kutokana na uzito wa tukio lenyewe.Katika kuwahi kujionea tukio live (sikwamba hawana Tv nyumbani) waingereza wengi wamekesha katika Tents nje ya jengo ambapo wawili hao wataoana mapema leo.

Katika tukio hilo ambalo litakua katika ulinzi mkali watu zaidi ya million moja wanatarajia kuhudhuria katika eneo hilo na watu Billion mbili wataona/sikia tukio hilo kupitia vyombo mbalimbali ikiwemo Live Tv,Internet,Radio etc.Habari zaidi zinasema wengine wata jiachia kwa party za mitaani katika kusherekea siku hii ya mapumziko wakati prince William anaoa  jijini London mapema leo. SI VIBAYA KWA WENYE MA HOTELI TANZANIA NA MAHALI PENGINE KUZINGATIA UMUHIMU WA SIKU  HII  KWA KUWABURUDISHA WATEJA WAO (WAINGEREZA) AMBAO KWA TANZANIA WAKO WENGI TU ILI WASIJIONE WAKO MBALI WAKATI WENZAO HUKU (UK)  WALA BATA SIKU NZIMA!

                               Mke na Mme watarajiwa Kate & William                                               

Wageni rasmi katika harusi hii ni 2000 na katika hali isiyo ya kawaida, pamoja na ukaribu uliopo kati ya UK na USA Rais Obama haja alikwa!! Kwa maana hio naye ataona kwenye Tv kama mimi (kama atakua na muda) hii kali  lol.

Kupata Ratiba ya Royal Wedding ingia hapa: http://www.theroyalweddingwilliamkate.com/the-wedding-day-schedule

Kuangalia ROYAL WEDDING LIVE ingia hapa: http://www.royalweddinglive.tv/kate-and-william-wedding-day/

No comments: