Kumezuka vurugu jijini London Uingereza baada ya raia mmoja kupigwa risasi na polisi.Vurugu hizo zilizuka baada ya polisi kuzuia maandamano ya amani na kuhoji kwanini raia Mark Duggan (29) aliuawa na polisi kwa kupigwa risasi? Tukio hilo lilitokea Tottenham Alhamis Tar 04 na Jumamosi ya tarehe 06/08/2011 ndipo vurugu zilipozuka eneo hilo na kusambaa miji kadhaa hapa England.
Mark Duggan,29 wakati wa uhai wake
Hali hiyo ya vurugu imeingia kwa kasi miji mingine kama Birmingham,Liverpool,Manchester na Bristol.Ukiachia mbali huyu jamaa kuwa chanzo maisha magumu,ukosefu wa ajira unaozidi kukua na ubaguzi wa rangi vimetajwa kuchangia vurugu kuungwa mkono kwa kasi.Waziri mkuu David Cameron aliyekua mapumzikoni Italy amelazimika kurudi kwani hali ni tete.Jana 08/08/2011 Birmingham palikua hapatoshi.
Polisi ambao walizidiwa nguvu wakiwa wanaangalia kinacho endelea kama kideo!
maduka,magari yalichomwa moto
Mtaani kulikua kama hivi
Jamaa wenye mask wakiiba dukani na kuvunja ATM machine na kuiba Pound!
Picha zote toka Aljazeera na BBC
Kwa habari zaidi soma HAPA na HAPA
No comments:
Post a Comment