09 August, 2011

WANAWAKE WADAIWA KUBAKA WANAUME!!!

Huko kwa Mugabe nchini zimbabwe kuna tuhuma za wanawake kuwabaka wanaume kwa makusudi .Ubakaji huo umedaiwa kukua siku hadi siku kwani kwasasa ni kila wiki lazima mwanaume abakwe!.Mkuu wa polisi jijini  Harare Angeline Guvamombe amesema “  wanawake wanao endesha magari ya kifahari huwapa wanaume lifti na kuwapulizia maji maji usoni yanayowafanya wasinzie na baadae kulazimisha kufanya nao mapenzi'' Kwa mujibu wa  the Herald  wiki mbili zilizo pita wanaume wawili walitekwa na kulazimishwa kufanya nao mapenzi chini ya usimamizi wa bunduki. Wakati katika tukio lingine wanawake watatu walimteka mwanaume wa miaka 30 na kumlazimisha kufanya nae mapenzi kwa siku 5!!.


Cha ajabu tangu ubakaji huo kuanza hakuna mtu amekamatwa kwa kosa hilo na polisi wamesema wanawake hawawezi shitakiwa kubaka kwani sheria ya Zimbabwe haitambui kama mwanamke anaweza mbaka mwanaume na hivyo mwanamke anayebaka anaweza shitakiwa tu kwa kumvamia mwanaume kwa nguvu (assault) na kupata adhabu ndogo ikilinganishwa na ile ya mwanaume kubaka.


Hii ni changamoto katika nyanja ya sheria kwani mabadiriko ya wakati yamebadirisha mfumo wa mahitaji.Je kwetu Tanzania hali ikoje katika maswala haya? Wanasheria tuambieni ili tujue mie nikibakwa nijue kama haki yangu ipo ama laa kwani kwa mpango huu hakika wanaume watakua hatarini kuambukizwa magonjwa ya zinaa bila kupenda!Kwa habari zaidi soma: HAPA 


No comments: