11 August, 2011

TANZANIA BILA UMEME/MAFUTA INAWEZEKANA??

Ilikua.........................

Heshima ikajengeka mjini na salamu zikatolewa kama hivi.........

Ghafla bin vuuu mara...........
Vidumu ndio mpango duh kweli Bongo Raha! hapo bado adha ya umeme,maji safi,foleni,stress binafsi n.k

Wauza wese nao wataka heshima!! sijui wanataka salamu kama hio ya Tanesco?.Hakika hivyo vituo vya mafuta  vingekua tu huku kwenye vurugu zilizo anza baada ya mtu mmoja tu kuuawa basi zingebaki historia,magofu ama kuchukuliwa mafuta yao kwa nguvu tena bure 'yaani take now don't pay later' kama ambavyo tutaona matukio zaidi yaliyo jiri hapa UK.Watu wamechoka na blah blah wakati maisha magumu.Siombei tufikie huko lakini huenda ndiko tunako elekea bila kujijua. Je viongozi wetu wanaliona hili? au wao haiwahusu? Nauliza tu!

2 comments:

Miss K. said...

Tatizo kubwa ni sisi wenyewe kuchagua mtu ambaye hakufanya lolote kwa kipindi cha miaka 5. Sasa naona tumempa nafasi ya kuonyesha jinsi gani hajali vilio vya waTz. Haiwezekani maendeleo bila ya maji, umeme na sasa mafuta. Unategemea watu waishi vipi? Halafu amekaa kimya kama kawaida yake ndo kwanza kasafiri kwenda nje.Watu hawawezi kuishi kwa vibatari hii ni karne ya 21. Kusema kweli sielewi kwanini yote haya yanatokea..

Rik Kilasi said...

Miss K Siasa ya Tanzania kuja kubadirika itachukua muda sana hasa ukizingatia kipindi cha kampeni wagombea humwaga mapesa raia na shida zake anasahau mateso yote anamchagua.Yale mapesa yatarudi vipi kama sio kususia miradi endelevu na ya umma na kua bize kurudisha mapesa?

Kweli kazi tunayo kama mambo yenyewe ndio haya kwani ni aibu ukitazama kama umeme unawaka kama 15% ya nchi nzima and yet mgao mkali sasa jiulize kama ungewaka nchi nzima nadhani mgao ungekua kwa mwezi umeme ungewaka mara1.Ni imani yangu changamoto zilizo ikumba serikali kipindi hiki zitaleta mabadiriko chanya katika utendaji ama uwajibikaji wa serikali