16 August, 2011

HIVI KWELI MAPENZI SUMU?

Kwa wale ambao wamekwisha chukua maamuzi magumu ya kuoa hasa miaka yasasa wanaweza kua na majibu  sahihi ya hili swali.Lakini pia katika harusi zote nilizo hudhuria hua sikosi kusikia ''MKAVUMILIANE NA KUHESHIMIANA'' hivi vitu viwili vikikosekana lazima ndoa iyumbe kwa namna moja ama nyingine.Hata hivyo ndoa sasa hivi hazidumu je tukubali kua mapenzi ni sumu?.Kimtazamo kama usemi huu una ukweli  kwa asilimia kubwa basi ishakua balaa!!

Mie nilikua nadhani ukiwa na mpenzi (Mke/Mme) basi ni raha kumbe inaweza kua kinyume chake.Na kwakua sasahivi ndio wanaita muda wa haki sawa,kwenda na wakati basi talaka ndio nje nje tujiulize kwanini?.Mbali na hio vijana sasahivi wanachelewa kuoa/kuolewa je tatizo ni nini?? Wengine wanasema ndoa ndoano je hii ni sababu ya ambao hawajaoa kutooa mapema?

Mtazamo wangu, kwakua imekua mila na desturi sehemu nyingi Africa hususani Tanzania toka zamani tumeona mwanaume ndio mtoa maumuzi ya mwisho (aka kichwa cha familia) si vibaya kwasasa mwanamke kushirikishwa katika maumuzi mbalimbali katika familia.Kusingizia haki sawa miongoni mwa wanawake na kujenga kiburi mwisho wake talaka.


Ni lazima kuheshimiana na kusikilizana kwa wapenzi/wanandoa (kama mnataka kufurahia).Mambo uliyofanya ukiwa pekee yako lazima uangalie kama yana mchango mzuri katika mahusiano kama sivyo basi achana nayo.Imekua utaratibu sasa hivi wapenzi kusema wanataka uhuru unakuta mtu kaoa/kaolewa na bado ana mawasiliano ya karibu na mpenzi wa zamani ya nini hasa?


 Hii tabia sio nzuri ndo mwanzo wa kupokelea simu chooni,kuzima simu ukiwa na wako,kuweka silent na kuwekeana password ambazo huongeza maswali ni je unaficha nini?? Mambo ya vidumu mpaka lini na magonjwa yaliyozagaa?? Nadhani hii ni moja ya sumu ya mapenzi, na kwanini tusiite mapenzi raha/matamu na maneno kama hayo kwa kuepuka hizo sumu ambazo ziko wazi?

2 comments:

H. J. Simaya said...

Wazee wetu wa jadi walifurahia mahusiano yao, na waliweza kuishi miaka mingi katika ndoa,... Ijapo kuwa sewezi kuhitimisha kwakusema hawakuwa na matatizo.Swali tulanalofaa kujiuliza ni kwa nini hawa wenzetu waliweza kukabiriana na karaha zote za mapenzi..
Jibu nadhani ni rahisi.. safari ya mapenzi, inahitaji upendo wa dhati..sio kudanganyana kati ya wapendanao, uvumilivu..hapa tunafaa kukumbuka kwamba sisi sote ni binadamu... we are prone to mistakes .. kukaa chini na kutafakari ni mambo yapi yanayoharibu mahusiano kati ya wawili wanaopendana na hatimaye kukubali kuwa na kiongozi katika ndoa,... jamani kama hutatuweza kufanya hivyo basi Goriati wa mapenzi hutuwezi kupambana naye..
Yakhe mmoja aliamba..'Nyakati hizi tuishizo sasa.. mwanzo wa mapenzi huwa ni mtamu kama asali... katikati ya mapenzi huwa ni mtamu kama limao...lakini mwisho wa mapenzi huwa mchungu kama shubiri (sumu ya mapenzi)
Hii ni kwa sababu watu siku hizi hawana nyenzo sahihi za kukabiriana na tatizo hili...

Rik Kilasi said...

Nadhani upo sawa Mr Simaya swala zima la mapenzi ya kweli kwa hali yasasa bado ni kitendawili wengi tunatamaniana tu na kudhani tunaweza ishi wote.Kuna watu wanaangalia mali,uzuri bila kujali tabia za mtu kwakujipa moyo labda 'atabadirika' (kama ana tabia mbovu) si wote wanaweza badirika

Nadhani ifikie wakati watu wajue mwenza wa kuoa/kuolewa naye lazima awe ni mwenye asilimia kubwa ya kuendana na mapungufu yake na si vinginevyo.Kupuuzia haya au kusema ngoja nikajaribu unaweza jikuta unajaribu watu kibao na umri unaenda na kila mtu atakuaona huna maana na hujatulia.Mbali na hilo kuna magonjwa yamezagaa,kwahio ni vizuri kuchagua aliye sahihi ili usijutie uamuzi wako hapo baadae japo hili zoezi ni gumu tukikumbuka kwamba tabia za binadamu hubadirika kuendana na mazingira na tukio kwahio inakua ngumu kumjua nani anaigiza na nani mkweli cha msingi ni kumshirikisha tu Mungu katika mchakato mzima wa kusaka mwenza wa ukweli sio muigizaji kwani sasa yanageuka kua maigizo vile japo si kwa wote!