19 May, 2011

VIJISENTI VINAPOSHINDWA KUKUSAIDIA..

Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss-Kahn ambaye pia ni mwanasheria,mwanasiasa na mwanauchumi wa kifaransa amewekwa jela Marekani kufuatia madai ya kutaka kumbaka mhudumu wa Hotel (Hotel Maid).Baada ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani kufuatia kitendo hicho bwana Strauss-Kahn kupitia mwanasheria wake aliomba aachiwe kwa dhamana ya (vijisenti)  Dollar Million moja ($1m) mahakama ilikataa dhamana hio na kumrudisha rumande.


                                       Aliyekua mkurugenzi wa IMF-Dominique Strauss-kahn 

Kufuatia skendo hio mkuu huyo wa IMF amelazimika kujiuzulu wadhifa wake ambapo Umoja wa nchi za Ulaya (EU) wamesha tangaza kinyang'anyiro na wagombea wa awali ni kama ifuatavyo:-

  • Mohamed El-Erian, Egypt

  • Stanley Fischer, Israel

  • Gordon Brown, UK

  • Kemal Dervis, Turkey

  • Peer Steinbrueck, Germany

  • Montek Singh Ahluwalia, India

  • Christine Lagarde, France

  • Agustin Carstens, Mexico

  • Trevor Manuel, South Africa

  • Axel Weber, Germany
  • No comments: