19 May, 2011

ETI JUMAMOSI TAREHE 21/05/2011 MWISHO WA DUNIA???!!

Imeripotiwa kutokea wahubiri wa kidini jijini New York-Marekani kufuatia wanacho dai mwisho wa dunia ni tarehe 21/05/2011 ambayo ni siku ya Jumamosi.Wahubiri hao ambao wamekua wakifanya kazi hio bila kuchoka wametoa vielelezo mbali mbali kuthibitisha tukio hilo.Zaidi wamedai tukio hilo si lazima litokee wakati mmoja duniani kote kufuatia kutofautiana masaa lakini lazima iwe tarehe iliyo tajwa!!

Ni matumaini yangu hayata tokea yale ya Kibwetere wa Uganda kuchoma moto waumini wake wanao sadikika  kufika 1000 ndani ya kanisa la '' Amri kumi za Mungu'' eti mwisho wa dunia umefika na kubaki yeye na bosi msaidizi wake  Bi Credonia Mwerinde nje mnamo Machi 17 mwaka 2000.Hata hivyo mpaka sasa haijulikani kama Kibwetere  na mwenzie wapo hai na polisi wa Uganda kwa kushirikiana na wale wa kimataifa (Interpol) bado wana mtafuta Kibwetere popote alipo Duniani. Pamoja na kua na maswali mia nane kidogo mie yangu macho!!

Kwa habari zaidi soma hapa:http://uk.news.yahoo.com/preachers-prophesying-end-world-york-000338169.html

Zaidi kuhusu Kibwetere soma hapa:http://www.culteducation.com/kibwetere.html

No comments: