06 May, 2011

AL-QAEDA WATHIBITISHA KUUWAWA KWA OSAMA

Habari zilizo jiri hivi karibuni toka kundi la kigaidi la Al-Qaeda ni kwamba kiongozi wao Osama Bin Laden ni kweli ameuawa na Marekani nchini Pakistan eneo la Abbottabad.Habari hizo zimenaswa kwenye mtandao unaosadikika kutumiwa  na kundi hilo wakidai shangwe za Marekani kwa kifo cha kiongozi wao kitageuka kua huzuni hivi karibuni.Hata hivyo kundi hilo limeahidi kuwepo kwa mashambulizi mapya kwa Marekani na washirika wake kusherekea miaka kumi ya mauaji ya 9/11 Marekani.Hio ni sambamba na kuishinikiza Pakistan kuandamana kwa kitendo cha Marekani kumuua Osama.


Katika upande mwingine Marekani imedai shambulizi la kumuua Osama limewawezesha kupata habari ambayo Osama ali rekodi siku chache baada ya kifo chake.Habari hio ilikua ni ya mashambulizi ya kulipua Reli na treni huko Marekani.


Kwa habari zaidi soma hapa: http://uk.news.yahoo.com/bin-laden-plotted-attack-us-trains-022222947.html


       na hapa                                  : http://news.sky.com/skynews/Home/World-News/Video---Osama-Bin-Laden-Barack-Obama-At-Ground-Zero-Amid-Pakistan-Compound-Raid-Story-Doubts/Article/201105115986145?lpos=World_News_Third_Home_Page_Article_Teaser_Region__4&lid=ARTICLE_15986145_Video_-_Osama_Bin_Laden%3A_Barack_Obama_At_Ground_Zero_Amid_Pakistan_Compound_Raid_Story_Doubts

No comments: