06 May, 2011

JOSE MOURINHO APEWA BAN YA MECHI TANO

Jose Mourinho (Meneja Real Mdrid)
Meneja wa timu ya Real Madrid Jose Mourinho apewa ban ya mechi tano ikiwa ni adhabu kutoka UEFA kufuatia kushangilia kinafiki baada ya kutolewa uwanjani mchezaji wa Real Madrid 'Pepe'  na baadae Wolfgang Stark  mwamuzi katika mechi hio  kali baina ya Barcelona na Real Madrid kumpa kadi nyekundu Jose ambaye alionekana kushangilia adhabu ya mchezaji wake.

Adhabu hio ni sambamba na faini ya Euro 50,000  kwa Jose Mourinho na 20,000 Euros kwa kilabu hicho kufuatia utovu wa nidhamu wa washangiliaji wa Real Madrid uwanjani siku hio ya mchezo ambapo Barcelona waliibuka kidedea kwa 2-0 usiku huo dhidi ya Real Madrid.Pepe mwenyewepia alipewa ban ya mechi moja na kwa upande wa boss wake (Mourinho) amesha tumikia adhabu hio kwa kuto hudhuria mechi moja na kilabu hicho kimedai kukata rufaa kwa adhabu  zilizo tolewa mapema iwezekanavyo.

zaidi soma hapa: http://www.skysports.com/story/0,,11833_6916716,00.html

No comments: