07 March, 2011

LIVE TOKA ENEO LA TUKIO..

Katika kupita pita kupata habari hapa na pale nikaja kutana na habari ya mada kuhusu  urembo wa wasichana wakitanzania dhidi ya wale wanaijeria kupitia http://u-turn.co.tz/index.php?start=10. post ya tarehe 01/03/2011. Mada hio iliambatana na pichaa kadhaa za wasichana wa kitanzania yamezaa maoni lukuki yaliyo katika mtindo wa kubishana/kujibishana tena kwa maneno makali. Mpaka sasa haijajulikana nani ameanzisha malumbano hayo makali  pamoja na kutuma picha kwa blogger aitwae Linda wa Nigeria.

Wengi wanasema pengine imekua gumzo kwa mshindi wa BBA (Kevin-Nigeria) kumuoa Mtanzania (Elizabeth) wakiuliza kwani Nigeria wasichana wazuri hakuna? kwenye comments za wanaijeria wakaka wanasema wadada wakitanzania hujipendekeza kwao kwa uzembe wakutaka vya bure na wao ndio wanawachukua ila si kwamba ndio wazuri.Mimi sijui ukweli ndio upi zaidi ya kusikia wasichana (Baadhi) wakitanzania kuwasifia wanaijeria ndio wanaume wa ukweli na wanajua kujali (mimi sina maoni juu ya hilo)

Ukisoma maoni yaliyo tolewa wameitukana hadi Tanzania kama nchi (Too bad) hasa katika swala zima la umasikini na kwamba wengi wetu ni vihiyo,washamba,lugha haipandi na masikini wakubwa.Hata hivyo wa kaka wa kinaijeria wamesema kuwa wasichana wao ni wazuri kupita wakitanzania ila kwakua hawa wa Tanzania ni cheap ndio huwachukua.Wakati huo huo wasichana wakinaija wamesema (kupitia maoni) kua huyo aliye olewa na mume wao (yaani kaka wa kinaija) basi watakula naye sahani moja!

Malumbano hayo ambayo hayana miguu wala kichwa yamezaa maoni mengi  kupita kawaida katika blog hio kwa kulaani hio mada ya kulinganisha kazi ya Mungu (ambayo siku zote haina makosa) na kupelekea kila mmoja kwa nafasi yake kujitetea  tena kwa hasira na Lugha kali.

Blog  hii inalaani yeyote aliyepelekea kuazishwa kwa mjadala huo duni na kutoa wito wa kutoa mada za kujadili mambo ya msingi na maendeleo na sio 'Urembo/beauty' ambao uko subjective kwa kiasi kikubwa kwani kila mmoja anaweza kuwa na mtazamo tofauti katika Urembo wahenga walisema 'Beauty is according to the eyes of the beholder'. Kwahio tujadili mambo mengine sio haya yanayo lete mabishano yasiyo na umuhimu.

 Sitaki kuongea mengi ili kuona mjadala ulivyokua na maoni ambayo mpaka naandika hapa yamefika 134 ingia hapa: http://lindaikeji.blogspot.com/2011/02/are-tanzanian-women-more-beautiful-than.html

Pia ukitaka ona post na comments za u-uturn  kuhusiana na mada hio hio na comments za watanzania ingia hapa: http://www.u-turn.co.tz/index.php/kwanza/1588-ohoooo-wanaigeria-wanatutafuta#JOSC_TOP

No comments: