Babu mmoja kwa jina Ambilikile Mwasapile (76) wa Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha amejipatia umaarufu wa ghafla baada ya kugundulika anatibu magonjwa lukuki ukiwemo UKIMWI.Babu huyo ambae inasaidikika ni mchungaji mstaafu wa kanisa la KKKT-Loliondo amesema mwanzo ilikua ni ndoto ambayo amekua akiiota toka mwaka 1991 ambayo Mungu amemuagiza aponye watu.Ndoto hio imejirudia rudia mpaka Augusti mwaka 2010 ambapo aliamua kuanza kutoa tiba rasmi kwa gharama ya sh.500 tu.
Mpaka sasa maelefu ya watu mbalimbali,vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake wamekuwa wakienda kwa mzee huyo kupata tiba na baadhi wamekili ni TIBA HALISI.Mpaka sasa ni kama kitenda wili machoni pa watu kila mtu akiuliza ni kweli au sio kweli.Kwenye mitandao mbalilimbali kama facebook,blogs,webisites na chatrooms gumzo ndo hilo japo bado hawaamini kama ni kweli na wanasema kama ni kweli na wao wataenda
Kwa walio ona foleni ni kubwa kupita maelezo katika kufata tiba hio ya asili na huenda babu huyo akavunja rekodi ya utojai tiba asili nchini Tanzania tena kwa muda mfupi. Kama utavyo ona picha hapo chini watu ni wengi sana kama nilivyozitoa Facebook.
Siku zote mimi huwa nasema kwa watu wa karibu UKITAKA KUJUA KAMA KUNA WATU WANAUMWA NENDA HOSPITALI NA UKITAKA JUA KAMA WATU WANAKUFA NENDA MAKABURINI.Bila hivyo hutajua labda kama anaye umwa ama kufa ni ndugu ama jirani au wale ambao utaona ama kusikia kupitia vyombo vya habari.
Msafara kwenda kwa babu
Babu akiwa amezungukwa na watu waliofata tiba pamoja na kushangaa
No comments:
Post a Comment