09 March, 2011

YALIYO JIRI-LOLIONDO                                                ITV  na Taarifa kuhusu kinacho endelea LoliondoHali livyo hivi sasa Loliondo kwa babu.

Hakika huyu babu anahitaji msaada wa haraka maana pamoja na watu kwenda wakitembea wenyewe, kuna wale wagonjwa walio bebwa ambao bila shaka hali zao sio nzuri.Si hivyo tu pia hali ya usalama kufuatia kugombea huduma kunaweza zua jambo lingine la hatari.Kila mtu anataka kuishi, kila mwenye mgonjwa angependa mgonjwa wake atibiwe mapema iwezekanavyo ila kwa uwingi huu wawatu hakika huyu babu hataweza kumudu akiwa hana msaada  wa ziada kwani watu hawataweza vumilia kulala nje kila siku.Si hivyo tu kuna wagonjwa ambao kwa msongamano huo wa watu lazima watapoteza maisha.Serikali ichukulie jambo hilo uzito wa ziada ikiwa ni pamoja na kuhakiki ukweli wa tiba hio. Ni hayo tu kwa leo.

No comments: