09 April, 2010

Helpful kids......

Ni vizuri sana na ni furaha kwakweli kuona mtoto wako anakusaidia kazi za nyumbani.Japo familia nyingi wanaonekana kusaidia kazi hizo ni wasichana. Hata hivyo wapo walio sikika wakilalamika kwanini watoto wakike ndio wafanye hizo kazi hususani wale wakusoma ambao wanahitaji pata muda wa kujisomea warudipo nyumbani! kama ilivyo ada kwa watoto wakiume ambao kazi za jikoni si kawaida kuona wakisaidia.(hii ni kwa watoto walio day) mie ningetaka kusoma boarding straight kama mambo yenyewe ndo hayo hehehe japo unakua unajifunza kazi za jikoni pindi utapoa anza maisha yako.

Mtu anaweza cheka hili jambo ila ni aibu kuna watu unakuta ashakua mtu mzima hajui hata kuosha sahani ama kijiko.Zamani kuna baadhi ya shule walikua wanafundisha cookery course ambayo sijawahi ona mtoto wa kiume anasoma (Late 90s pale Njombe secondari maarufu kama NJOSS) Ila sina shaka na wale ambao wameishi ulaya maana ifikapo muda wa kurudi makwao wanakua wanakaribia kua ma-chef kabisa maana huku lazima ujue kupika ama sivyo utaishia kula burger na junk food ukaharishe vizuri nyumbani kwako hahahhahha.... Well, nilichotaka kusema hapa ni kua makini na mtoto anayekusaidia na kile anacho kusaidia vinginevyo haitakua kusaidia bali uharibifu wa vitu vyako kama ionekanavyo kwa hio picha. yaani sina mbavu na hio picha naona mama mtoto ashituka na kushindwa kushangaa....

No comments: