21 July, 2011

KISONONO SASA HAINA TIBA!!!!!!!!

Kuna habari kuwa wana sayansi  huko Japan wamegundua kuwepo kwa jamii ya gonorrhea (kisonono) ambayo haitibiki kwa dawa zote ambazo awali zilikua  zikitibu gonjwa hilo.Jamii hio iliyopewa jina la H041 imewaacha madaktari midomo wazi kwani dawa zilizopendekezwa hazitibu tena na kuwafanya wajaribu kutumia dawa zingine ambazo hazikujaribiwa kutibu ugonjwa huo ili kutafuta suluhu ya ugonjwa huo ambao umedaiwa kua tishio jipya idara ya afya siku za usoni kama tiba haitapatikana.


Gonorrhea hapa Uingereza ni ugonjwa uliozagaa sana pamoja na Chlamydia (klamidia) ambayo yote ni magonjwa ya zinaa maarufu na umaarufu wake unakua siku hadi siku ukiumwa daktari hata hashangai!!.Magonjwa haya unaweza yapata kwa kufanya mapenzi bila kinga na muathirika.Kwa maana hio mambo ya kusema huniamini na blah blah kama hizo LAZIMA TUZIACHE VINGINEVYO HALI ITAKUA MBAYA NA HUO UTAKUA MKATABA WA MIONDOKO YA BATA WAKATI WA KUTEMBEA (usicheke ila ndivyo ilivyo ukiupata)


Kibaya zaidi ukishapata haya magonjwa uwezekano wa kupata HIV/AIDS na magonjwa mengi ya zinaa ni mkubwa.Na kujua kama umeupata inachukua siku 5 hadi 30  dalili ni pamoja na kusikia maumivu unapokojoa (kwa wanawake/wanaume), kutokwa usaha wa njano kwa wanawake na kuvimba korodani kwa wanaume.Aidha kwa wanawake wakati mwingine hakuna dalili yoyote ukiupata zaidi ya kua na uwezekano mkuwa  wa kuharibika mimba mara kwa mara, kuzaa kabla ya siku au ugumba wakati kwa wanaume inaweza pelekea kansa  ya kibofu (prostate cancer).


Kwahio tucheze salama ndugu zangu!


Zaidi kwa lugha ya kiingereza soma HAPA na HAPA 

No comments: