21 July, 2011

ATI UTANI KWA WAHEHE....JE NI SAWA?

Ukiangalia kwa haraka unaonekana kama ni utani lakini ukitafakari huu ni uchokozi wa maksudi katika kubeza makabila.Leo katika blog ya rafiki yangu Mwanasosholojia nimekuta utani kuhusu kabila la Wahehe ambao si vibaya wasomaji wake tukafaidi na nikaona si vibaya na sisi hapa kuona mawili matatu.Kiukweli nimecheka sana japo sijaufurahia utani kama huu kwani unanigusa kiasi fulani na kinacho kera zaidi mtu ukimwambia unatoka Iringa cha kwanza kusema ni ''eeh nisikuuzi usije jinyonga bure'' au ''eheee kwahio unakula mbwa??''

Kiukweli sijui kama Wahehe wanakula mbwa maana sina ushahidi ila nasikia tu watu wakisema.Hua pia najiuliza kama wahehe ndio wanakula mbwa kwanini iwe wote watokao Iringa wahusishwe kubezwa kiasi hiki? Iringa kuna makabila mengi yakiwemo Wakinga,Wabena,Wahehe,Wapangwa n.k. No offense intended kama kuna mhehe unasoma hii habari labda niulize hivi kweli Wahehe mnakula mbwa??   Yaani hii chini ya mshale
                                  Nataka kujua tu msini elewe vibaya!

Swala la kujinyonga (suicide) lipo kila mahali kwa makabila yote mpaka wazungu wanajinyonga sasa sijui nao ni Wahehe?.Mtazamo wangu hili linaweza kua la kihistoria zaidi ukizingatia aliyekua Chief wao Mkwawa alijinyonga ili asitiwe mikononi mwa Wajerumani akiwa hai.Lilikua jambo la kishujaa zaidi ambalo pengine ndio chimbuko la mwendelezo wa kujinyonga baina ya Wahehe kwani pengine ni ushujaa kufanya hivyo.Lakini mpaka sasa si Wahehe peke yao ndio wanajinyonga ni mtu yeyote bila kujali kabila anaweza jinyonga kwa sababu zake binafsi au kutokana na jamii inayomzunguka,matatizo n.k.Well ni mtazamo tu tujiunge na tangazo hapa chini kwa imani kua ni UCHESHI TU NA SI VINGINEVYO!!


TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)

Kinatangaza kozi za mwaka 2011/2012 kama ifuatavyo,1.Kugema ulanzi miezi 6
2.Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9;  3.Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8;  4.Kuongeza hasira miezi 10-12Atakae jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.

ASANTE KAKA MWANASOSHOLOJIA,KWA HABARI ZAIDI MTEMBELEE HAPA

5 comments:

Mwanasosholojia said...

Ha ha ha!Kaka Kilasi (Mwa-Kilasi??:-))mbona kama na wewe "unaka-hasira" (joke tu kaka!)Dhana ya utani ni pana sana. Na kama ulivyosema, utani upo katika makabila mengi sana ya Tanzania. Kuna utani ambao una mantiki na mwingine sasa unakuwa kero. Ninachojifunza ni kuwa mara nyingi ni kuupuuzia na endapo mtaniaji anagundua kuwa unakukera, kuna wengine wanafanya makusudi na kuzidi kutania. Hii pia hutokea sana kipindi cha misiba, na hata kusababisha mitafaruku mbalimbali kati ya wafiwa na wataniaji.

Kwa kuwa suala hili limo ndani ya tamaduni za makabila yetu, sidhani kama ni rahisi kufutika. Linaendelezwa kila siku kwa simulizi mbalimbali na matukio. Ni kuvumiliana na kuonesha kutojali ili mtu akigundua hujali, anapotezea pia. Sirika ya binadamu siku zote huwa ni kuona mwenzake ana-react vipi. Shukrani sana kwa kuchangamsha mada hii kaka yangu!Peace and love!

Rik Kilasi said...

Hujakosea kaka Mats Mimi ni mwagito aka Mwakilasi hahaha.Kiukweli niliona nichangamshe mada maana ni kweli utani wa makabila upo sana ila huu wa watu wa Iringa nadhani ni common kwa kila mtu sasa maana unaweza ulizwa hapa Tanzania unatokea wapi ukisema Iringa tu swali linalofata ni je unakula mbwa? au wekeni kamba mbali asije jinyonga huyu hahhaha

Nakubaliana na wewe ni kupuuza tu utani wa hivi after all haupunguzi personality ya mtu na ni kweli utani unaendelezwa na huu wa Iringa sidhani kama utakuja kufutika mie hua nacheka tu kwakweli.Na kuna watu wanadhani Iringa wako Wahehe peke yao ndio maana nikataja pia Wabena, Wakinga,na Wapangwa ambao kwa bahati mbaya katika utani nao ni Wahehe pia kwakua wanatoka Mkoa wa Iringa.

Ila mie langu moja tu Wahehe wangetuambia ukweli wa huu utani japo tujue kama unaendana na ukweli hata kama haisaidii hata tukijua ukweli halisi lakini simbaya kujua

Nimekupata Mwanasosholojia mada hii iko hot jamaa walivyo itengeneza utadhani advert ya ukweli sasa nilipofika kwenye kipengele cha kugema ulanzi ndio nikajua huu utani na kuangua kicheko peke yangu.Nimekubali ubunifu wa huu utani lol

emu-three said...

UTANI kama sio MTANI, utaona ni kitu cha ajabu sana, na wakati mwingine utawaoana wahusika kama sio watu wasiofikiria, mfani mtu anang'ang'ania maiti eti asipolipwa kitu fulani hamuachii...wakati mwingine naona kama sio vitu vyenye manufaa kwa jamnii, lakini wenyewe wanaohusika wanaona ni jambo la kawaida, kwani leo kwake kesho kwa mwingine,
Lakini mimi kwa ujumla SIPENDEZEWI na utani hasa kipindi cha msiba, nafikiri sehemu kama ile ni ya kumuombea aliyetangulia mbele za haki na kuwafariji wafiwa, sio sehemu ya UTANI....Ni nionavyo mimi!

Rik Kilasi said...

Kaka emu-three nashukuru kwa mchango wako...nikweli kabisa utani kama sio mtani ni tatizo japokua tuna mitazamo tofauti katika kuupokea utani.Kwa maana hio kuna ulazima wa kujua unamtania nani na wapi na uwe tayari kwa matokeo ya utani huo bila kujali yatakua mazuri au mabaya.Kuna watu hawajui utani sasa ukimtania kuna uwezekano wa kusababisha mtafaruku.

Tukiangalia upande mwingine utani maeneo ya misiba binafsi naona sio mahala pake kwa namna yeyote ile.Utani tufanye maeneo mengine sio msibani

Anonymous said...

haha usisahau na kudua je?