14 October, 2011

MONEY vs HUMANITY


Nionavyo mimi pesa na utu wa mtu ni vitu viwili muhimu katika maisha ya kila siku, bahati mbaya siku zinavyo zidi kwenda uwepo wa pesa umekua na maana zaidi kuliko utu wa mtu.Kwanini? Mtu anaweza muondoa uhai mwenzie kisa anataka kupata pesa..Mtu yupo tayari kutafuta pesa hata kwa gharama ya maisha ya mtu mwingine.Sasa hivi imekua kawaida mtu ukisema kitu kama huna pesa basi husikilizwi kama umeongea cha maana.Aidha ukiwa na pesa unaweza fanya chochote kihalali au kinyume chake bila wasiwasi kwani pesa itakulinda.Hii ni sifa kubwa katika nchi zinazo endelea japo hata zilizo endelea kuna nafasi ya pesa lakini utu wa mtu una maana zaidi na hivyo pesa haiwezi kukulinda unapo hatarisha utu wa mtu kwa kutumia pesa zako.Je nchi yetu Tanzania inaona hili?


Ukitaka kuona kama pesa inamaana zaidi angalia picha hapo juu, sasahivi kuna maelfu ya watu Somalia na nchi jirani wakiwa na janga la njaa, maisha ya watu wengi yapo hatarini na muamko wa watu kutangaza janga hilo ni mdogo sana kulinganisha alipo kufa mwanzilishi wa kampuni ya Apple ambapo kila mtu ameonyesha kuguswa naye kwa namna moja ama nyingine.Je ni kwasababu alikua na pesa?, alitoa ajira nyingi? katoa bidhaa inayopendwa? mbunifu wa kihistoria katika maendeleo ya teknolijia?.jibu linaweza kua ni ndio lakini kwanini watu hawaguswi na hawa watu wanaokufa kila siku kwa kukosa chakula? ajali za kizembe kama zile za kuzidisha mizigo kwenye vyombo vya usafiri kwa manufaa ya watu fulani?.Je ni lini utu wa mtu utathaminika?

No comments: