14 October, 2011

LEO NI SIKU NA MWEZI AMBAO BABA WATAIFA ALIIAGA DUNIA


Julius Kambarage Nyerere (13 April 1922 – 14 October 1999)

LEO TAREHE 14 MWEZI WA 10 NI SIKU NA TAREHE AMBAYO TUNA ADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.SIKU HII NI SIKU MUHIMU KITAIFA NA PENGINE KIMATAIFA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA.KATIKA KUMBUKUMBU HII NI VEMA SERIKALI NA WATANZANIA KWA UJUMLA KUKUMBUKA MAMBO MUHIMU AMBAYO MWALIMU ALIKEMEA KW ANGUVU ZAKE ZOTE.MFANO WA MAMBO HAYO NI RUSHWA (CORRUPTION) MAARUFU KAMA KITU KIDOGO.

RUSHWA IMEKUA KAMA  MCHEZO AMBAO UMEZAGAA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA.SASA HIVI HATA UKITAKA HUDUMA YA AFYA YA HARAKA NI LAZIMA UTOE KITU KIDOGO.HUDUMA YA BURE BILA KITU KIDOGO HUWEZI PATA KWA MUDA UNAOTAKIWA.MCHEZO HUU MCHAFU UMEKUA KWA KIASI KIKUBWA KIASI KWAMBA KUNA WATANZANIA WANA AMINI BILA RUSHWA HUWEZI FANYA LOLOTE.

MADHARA YA RUSHWA NI PAMOJA NA KUTO KUWAJIBIKA KWA VIONGOZI WETU,UONGOZI USIO WA SHERIA,MAADILI WALA HAKI,AJALI,VIFO,MAENDELEO DUNI,HUDUMA MBOVU KWA JAMII MFANO HUDUMA ZA AFYA,ELIMU,BARABARA  N.K.ITAMBULIKE WAZI KATIKA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU KUA RUSHWA BADO NI ADUI MKUBWA ALIYEKOMAA NA KUIDIDIMIZA TANZANIA KATIKA NYANJA ZA KIUCHUMI,KIJAMII,KISIASA NA KIUTAMADUNI.TAASISI YA KUPAMBANA NA KUZUIA RUSHWA (TAKUKURU) IWE CHOMBO HURU NA CHENYE NGUVU KUWAJIBISHA WATUHUMIWA WA RUSHWA WANAPO BAINIKA BILA KUJALI NANI,CHEO,DINI WALA KABILA.ITAKUA HAINA MAANA KILA SIKU TUWE TUNASIKIA TAKUKURU WAMKAMATA  KAMANDA FEKI HUKO SIJUI WAPI!


MANENO HAYA YA MWALIMU YAPO AU HAYAPO? KAMA YAPO MBONA HATUONI WALIO KULA FIMBO 12 NA KUWAONYESHA WAKE ZAO WAKIWA WANATOKA JELA?.RUSHWA NI ADUI MKUBWA WA HAKI!


SOMA ZAIDI HAPA KUHUSU HISTORIA YA MWAL.NYERERE

No comments: