04 August, 2011

TUSIFIKIE TU HATUA HII .....ha ha haa !!!

Kufuatia sakata la kufukuzwa wabunge  toka mjengoni katuni hapa chini imenifurahisha sana kwa namna ujumbe ulivyofikishwa.Sasa tukifikia hatua kama hii sipati picha Bunge litakuwaje.Nadhani mchora katuni  ameonyesha  dawa ya uonevu ipo jikoni ipo siku utapatiwa suluhu ya namna hio ama inayoendana ili kwenda sawa ama kukomesha hali hio kabisa.Tujiunge ha ha haaaa!!! yani sina mbavu.Hongera Abdul
                                      Kesho kutwa!!!!?

Sasa hii ya hapa chini sijui wanamfurahisha nani? Kama bajeti haifai kwanini uipitishe? Huyu ndio mwakilishi wa mpiga kura!! Je tuseme wabunge wa namna hii hawajui majukumu yao bungeni?? Nadhani wabunge wa namna hii ndio wafukuzwe bungeni hawana faida na mwisho wataishia kulala tu wakati mjadala ukiendelea!
                          Kuna mwenye majibu swali ndio hilo, sema usikike!

4 comments:

emu-three said...

Mkuu tunaomba tusifikie huko...hahaha kweli mchoraji kafkisha ujumbe

Mwanasosholojia said...

Ndiko tunakoelekea kaka, uwezekano wa wabunge kupigana ngwala siku chache zijazo upo...:-)

Rik Kilasi said...

Yaani emu-three nilicheka sana nilipoona hii katuni ujumbe kafikisha.Tukienda katika maisha ya kawaida zamani nilikua najiuliza kwanini vijana maeneo fulani wanapenda kuwa mabaunsa siku hizi hata wanajiunga na vikundi vya karate baadae nikaja kujua uonevu ndio kitu kimewasukuma vijana mbalimbali kufanya hivyo ukiachia mbali wengine kutaka watoke bomba, hali imekua tofauti kwa wengine maana ukiona misuli tu unamuogopa!

Rik Kilasi said...

Mwanasosholojia mie macho yangu tu nasubiria kuona hahaha. Na ikitokea nitafurahi kuona hata wanaolala bungeni wamepokea vichapo lol