25 July, 2011

MADUKA YA BIDHAA FAKE ZA APPLE YAFUNGWA

Nilikua nashangaa pamoja na vitu vya Apple kuwa gharama lakini speed ya utumiaji imekua kubwa kutokana bei kua rahisi kwa baadhi ya vitu kumbe kuna Wachina walikua waki supply fake apple products kimya kimya huko Kunming city ambako serikali ya China imewashitukia na kufunga hayo maduka mara moja.


Sasa najiuliza hivi sisi tunashindwaje kuwa na serikali kama ya Wachina?  Bidhaa fake kila mahala na mbaya zaidi zote ni imported  na TBS tunayo!!!! Hapo hatujajua viwango vya bidhaa ambazo ni made in Tanzania!.Yaani nawaza tu kwa sauti bila kupata majibu wachina waliopo bongo wanauza tv na vitu vingine fake watafungiwa lini maduka yao? Sasa hivi ukinunua hata simu Guarantee unaambiwa ni 2 weeks!!. Wenzetu mfano hapa UK simu ina Guarantee kuanzia  mwaka mmoja na vitu vingine miaka 3 na  kuendelea na ni Made in China.Sasa inakuwaje Bongo iwe 2 weeks?

Kwa habari zaidi ingia HUMU

21 July, 2011

ATI UTANI KWA WAHEHE....JE NI SAWA?

Ukiangalia kwa haraka unaonekana kama ni utani lakini ukitafakari huu ni uchokozi wa maksudi katika kubeza makabila.Leo katika blog ya rafiki yangu Mwanasosholojia nimekuta utani kuhusu kabila la Wahehe ambao si vibaya wasomaji wake tukafaidi na nikaona si vibaya na sisi hapa kuona mawili matatu.Kiukweli nimecheka sana japo sijaufurahia utani kama huu kwani unanigusa kiasi fulani na kinacho kera zaidi mtu ukimwambia unatoka Iringa cha kwanza kusema ni ''eeh nisikuuzi usije jinyonga bure'' au ''eheee kwahio unakula mbwa??''

Kiukweli sijui kama Wahehe wanakula mbwa maana sina ushahidi ila nasikia tu watu wakisema.Hua pia najiuliza kama wahehe ndio wanakula mbwa kwanini iwe wote watokao Iringa wahusishwe kubezwa kiasi hiki? Iringa kuna makabila mengi yakiwemo Wakinga,Wabena,Wahehe,Wapangwa n.k. No offense intended kama kuna mhehe unasoma hii habari labda niulize hivi kweli Wahehe mnakula mbwa??   Yaani hii chini ya mshale
                                  Nataka kujua tu msini elewe vibaya!

Swala la kujinyonga (suicide) lipo kila mahali kwa makabila yote mpaka wazungu wanajinyonga sasa sijui nao ni Wahehe?.Mtazamo wangu hili linaweza kua la kihistoria zaidi ukizingatia aliyekua Chief wao Mkwawa alijinyonga ili asitiwe mikononi mwa Wajerumani akiwa hai.Lilikua jambo la kishujaa zaidi ambalo pengine ndio chimbuko la mwendelezo wa kujinyonga baina ya Wahehe kwani pengine ni ushujaa kufanya hivyo.Lakini mpaka sasa si Wahehe peke yao ndio wanajinyonga ni mtu yeyote bila kujali kabila anaweza jinyonga kwa sababu zake binafsi au kutokana na jamii inayomzunguka,matatizo n.k.Well ni mtazamo tu tujiunge na tangazo hapa chini kwa imani kua ni UCHESHI TU NA SI VINGINEVYO!!


TANGAZO KWA WAHEHE WOTE:
Chuo kipya kabisa cha Kihehe kimefunguliwa Kihesa, Iringa.(HEHE SKILLS AND TECHINICAL COLLEGE OF LIFE)

Kinatangaza kozi za mwaka 2011/2012 kama ifuatavyo,1.Kugema ulanzi miezi 6
2.Kusokota kamba za kujinyonga miezi 9;  3.Kuchagua mbwa anaefaa kuliwa na mapishi yake miezi 8;  4.Kuongeza hasira miezi 10-12Atakae jiunga mapema atapewa kozi ya upishi wa Mkunungu pamoja na uoshaji wa Mbeta.

ASANTE KAKA MWANASOSHOLOJIA,KWA HABARI ZAIDI MTEMBELEE HAPA

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA ATOA UFAFANUZI SWALA LA UMEME

KUSIKILIZA UFAFANUNUZI WA TATIZO LA UMEME TANZANIA KUTOKA KWA MHESHIMIWA RAIS MH JAKAYA MRISHO KIKWETE FATA LINK HAPO CHINI ALIVYO HOJIWA NA MWANDISHI WA BBC BWANA OMAR MUTASA.RAIS ANASISITIZA WATANZANIA MUWE NA SUBIRA SERIKALI INAFANYA JITAHADA KUBWA LAZIMA WATU WATAMBUE NA KAMA KUNA MTU ANA MAARIFA YA HARAKA KATIKA KUTOA UFUMBUZI WA UMEME BASI AYATOE SERIKALI ITAYAFANYIA KAZI.


ZAIDI SIKILIZA RAIS AKIFAFANUNUA KUHUSU UMEME KWA KUBONYEZA HAPA





KISONONO SASA HAINA TIBA!!!!!!!!

Kuna habari kuwa wana sayansi  huko Japan wamegundua kuwepo kwa jamii ya gonorrhea (kisonono) ambayo haitibiki kwa dawa zote ambazo awali zilikua  zikitibu gonjwa hilo.Jamii hio iliyopewa jina la H041 imewaacha madaktari midomo wazi kwani dawa zilizopendekezwa hazitibu tena na kuwafanya wajaribu kutumia dawa zingine ambazo hazikujaribiwa kutibu ugonjwa huo ili kutafuta suluhu ya ugonjwa huo ambao umedaiwa kua tishio jipya idara ya afya siku za usoni kama tiba haitapatikana.


Gonorrhea hapa Uingereza ni ugonjwa uliozagaa sana pamoja na Chlamydia (klamidia) ambayo yote ni magonjwa ya zinaa maarufu na umaarufu wake unakua siku hadi siku ukiumwa daktari hata hashangai!!.Magonjwa haya unaweza yapata kwa kufanya mapenzi bila kinga na muathirika.Kwa maana hio mambo ya kusema huniamini na blah blah kama hizo LAZIMA TUZIACHE VINGINEVYO HALI ITAKUA MBAYA NA HUO UTAKUA MKATABA WA MIONDOKO YA BATA WAKATI WA KUTEMBEA (usicheke ila ndivyo ilivyo ukiupata)


Kibaya zaidi ukishapata haya magonjwa uwezekano wa kupata HIV/AIDS na magonjwa mengi ya zinaa ni mkubwa.Na kujua kama umeupata inachukua siku 5 hadi 30  dalili ni pamoja na kusikia maumivu unapokojoa (kwa wanawake/wanaume), kutokwa usaha wa njano kwa wanawake na kuvimba korodani kwa wanaume.Aidha kwa wanawake wakati mwingine hakuna dalili yoyote ukiupata zaidi ya kua na uwezekano mkuwa  wa kuharibika mimba mara kwa mara, kuzaa kabla ya siku au ugumba wakati kwa wanaume inaweza pelekea kansa  ya kibofu (prostate cancer).


Kwahio tucheze salama ndugu zangu!


Zaidi kwa lugha ya kiingereza soma HAPA na HAPA 





11 July, 2011

NILICHOGUNDUA:UDANGANYIFU SIMU ZA MIKONONI

Baadhi ya hii mitandao ya simu za mikononi na nyumbani ni wezi kuliko tunavojua,hivi inawezekanaje unipigie simu na kuacha ujumbe wa promotion  za kampuni nizisikilize kwa gharama zangu? As if hio promotion ni lazima kuisikiliza!! yaani usipo pokea simu wakipiga wanakuachia ujumbe wa sauti ambao kuusikiliza unakatwa salio.Hata hivyo wanaotupigia simu toka nyumbani bongo tunashukuru kutupigia ila kama mtu hapokei acha ujumbe.Unakuta mtu kaacha voicemail hajaongea chochote wakati mie nasikiliza hio voicemail na nakatwa salio.


Anyways tuache hio mimi binafsi ni Tomaso haswaa na nimejaribu kutumia mitandao mingi kwa kufuata masharti ya mtandao wa simu nikitaka kupiga simu bongo lakini ukweli ni kwamba matangazo tunayo ona ni tofauti na hali halisi mfano juzi juzi nimejiunga na mtandao mmoja hapa Uingereza matangazo yao ni kwamba ukipiga Tanzania ni pence 1 kwa dakika nimetumia pound 5 na simu imekata chini ya dakika 25!!!. Leo tarehe 11,July 2011 nimekutana na Tangazo la kampuni hio hio  linasema kupiga simu Tanzania ni 10 pence kwa dakika nikafungua ukurasa wao kuhakiki ukweli  nilichokuta sikuamini macho yangu DAKIKA 1 NI  PENCE 19 NA SIO 10!!!.
                                             Tangazo lao la leo
Kwa mujibu wa tangazo lao la kwanza kama kupiga simu Tanzania ni pence moja kwa dakika inamaana nilitakiwa kupata dakika 500  kwani Pound 5 ni sawa na pence 500 sasa nikawa najiuliza mbona imekata mapema?  Nilichogundua ni kwamba dakika moja wanakata pence 20 na sio penny 1 kama tangazo linavyosema ..hio 20 ukiizidisha na dakika 25 unapata pence 500. Ina maana kama sasa imekua 10 pence kwa dakika basi ni dakika 50 kupiga Tanzania kwa Pound 5. Ila tangazo linakinzana na ukweli kwa maana ya viwango walivyopanga ukipiga simu Tanzania. kwa wale tunaopenda kupiga simu bongo kua makini na hii


Ukienda kwenye mtandao wao kuona bei halisi unakuta habari tofauti angalia mwenyewe hapo chini

PAYG Rates

International PAYG Rates
Select your destination to check the rates.
Destination 
Rates
Landlines5 pence per minute
Mobiles19 pence per minute
SMS10 pence  
READ MORE

10 July, 2011

SUDAN KUSINI YAWA TAIFA JIPYA AFRICA

                                             Raia wa Sudan kusini wakisherekea uhuru
Sudan ilikua ni nchi ambayo imekua na mvutano na mapigano ya hapa na pale kati ya Sudan  kusini na kaskazin kwa muda mpaka Sudan ya kusini ilipoamua kujitenga na kujiita Taifa linalojitegemea japo halikutambulika na Umoja wa Mataifa (UN) ama Umoja wa Africa (AU).Hatimaye mnamo July 9,2011 Sudan ya kusini imetambulika na Umoja huo kama taifa huru na kufanya bara la Africa kua na jumla ya nchi 54.


 Kushoto ni Rais wa Sudan kusini Jenerali Salva akiwa na Rais wa Tanzania  Dr Jakaya Kikwete katika hafla ya uhuru wa Sudan Kusini
Kutambulika kwa uhuru wa Sudan ya kusini ni njia moja wapo kuzuia umwagaji damu uliodumu kwa muda mrefu ambapo UN na AU zimeridhia na kutambua hatua hio kama njia ya kuzuia machafuko zaidi..Ripoti ya BBC inaonyesha takribani watu Million moja na nusu wamepoteza maisha.Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alikua moja ya viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za uhuru mjini Juba ambapo Jenerali Salva Kiir Mayardit ndio Rais wa kwanza wa Sudan ya Kusini.Ujumbe wa umoja wa mataifa ulikua ni kulitambua Taifa hilo jipya na kushirikiana nalo japo changamoto ni nyingi hasa kuwepo kwa vikundi kadhaa vya waasi, elimu duni na mengineyo (BBC).


Kwa habari zaidi SOMA HAPA




05 July, 2011

ATI NIMETUNUKIWA!!!!

HAWA WEZI WA MITANDAONI WANANIACHA HOI JUZI NIMEPATA EMAIL ETI NIMESHINDA MAMILLION YA POUND TOKA TRIPOLI, SASAHIVI NIMEPATA TOKA MISRATA HUKO HUKO LIBYA HATA SINA MBAVU.......SOMA MWENYEWE HAPA CHINI ILI USIIBIWE MAANA WAPENDA MITEREMKO UNAWEZA DHANI DILI UKAFANYA KIMYA KIMYA KUMBE UNAIBIWA NA UKISHAIBIWA INABAKI KUA SIRI YAKO!!:



Dear Friend

I am Dr. Zubaru Zalani Independent Non-executive Director of Misrata People’s jamariya Bank, Libya. I have a transaction of ($41m)Dollars.

To bring to your attention if only you would be interested and willing to assist me move the fund to your destination,

Note / Every Financial institutions have been paralysed in the country at the moment but I have a way of moving the fund out of Libya, if you indicate your full interest. Contact me with your infomations so that we can proceed the deal immediately

Please view this website on what is going on (http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-13767462)

Your Full name........................................................
your Private telephone number..................................
Your Country of origine.............................................
Your Occupation.....................................................
Your Sex.............................................................
Your Age..............................................................

Yours Sincerely

Dr. Zubaru Zalani

Misrata Libya

02 July, 2011

HATIMAYE ALIYEKUA MKURUGENZI WA IMF AACHIWA HURU

                                Aliyekua boss wa IMF akiwa anafuraha baada ya kuachiwa huru


Aliyekua  mkurugenzi wa shirika la fedha duniani (IMF) bwana Dominique Strauss Kahn (62) aachiwa huru baada ya madai ya kutaka kubaka muhudumu wa Hotel  May 14,2011  jijini New York kutiliwa mashaka.Uamuzi huo umetolewa na mahakama iliyokua ikisikiliza kesi hio Ijumaa ya tarehe 1 July (jana) baada ya kufanya uchunguzi wa madai na kukuta mdai amedanganya na  kuchanganya maelezo kitu kinacho ashilia ni mwongo na kumfanya mdaiwa kuachiwa huru bila dhamana na kuondolewa vikwazo vyote.Aidha kesi hio ambayo inaelekea kufutwa haina haraka ya kusikilizwa tena kama mwanzo na mdaiwa ameombwa kuhudhuria mahakamani mara kesi itapo tajwa!.


Kesi zote zingekua zinasikilizwa haraka hivi watu wasingekesha na kupata shida mahabusu tena kwa muda mrefu au huyu kwasababu ana vijisenti?


Kwa habari zaidi SOMA HAPA