15 June, 2011

KWIKWI ZA FACEBOOK...Kwa sisi wapenzi wa 'Facebbok' kuna taarifa kwamba  watu wengi wameanza kufunga akaunti za facebook kwa sababu mbalimbali ambazo hazija wekwa wazi kwa sasa.Ripoti ya awali inaonyesha watumiaji wakuu wa facebook ni wa hapa Uingereza na Marekani ambapo kwa Uingereza nusu yao wamefungua akaunti facebook kwa makadirio ya watu million 30-34 na mpaka sasa akaunti 100,000 zimefungwa wakati Marekani akaunti zimepungua kutoka Million 155.2 mpaka 149.4.Hali kadharika Canada zaidi ya akaunti Million 1.5 zimefungwa. 


Wengine wamefunguka kwamba ----->


        Je wewe unasemaje facebook is like-------------------------------!!!?    


Cha ajabu kabisa wakati akaunti zikifungwa nchi zilizo endelea na zenye watumiaji wakubwa hali imekua kinyume na nchi zinazo endelea kwani watu wanajiunga na mtandao wa facebook kwa wingi iwezekanavyo na kuanika habari zao huko bila kujali kama kuna madhara yoyote.Hali hio imepelekea idadi ya watumiaji facebook kufika karibia Million 700.Kwa mujibu wa ripoti hio watu wanafunga akaunti facebook kwa sababu  za kiusalama zaidi kwani ulinzi wa taarifa wanazo weka facebook hauna guarantee mtu anaweza iba na kufanya chochote atakacho kwa mazuri au mabaya.Hivyo wapenzi  na watumiaji wa facebook kumbukeni kufanya security na privacy settings kulinda akaunti zenu ili nanyie msiwe waathirika wa  hujuma zinazo endelea kwenye hicho kitabu cha sura maarufu kama facebook


Kwa habari zaidi bofya HAPA
No comments: