03 May, 2011

NANI ALAUMIWE??

Hivi mwanafunzi kama huyu akifeli ata mlaumu nani?. kweli walimu wetu wana kazi kubwa sana kama mambo yenyewe ndio haya.Hivi kwani mtu huwezi zima simu ukiwa darasani ok, kuzima ngumu weka silent basi kwani simu kuita darasani mbali na kukupotezea muelekeo katika kipindi inaharibu utulivu na mwendelezo wa kipindi darasani.Mie naona wanafunzi wa aina  hii aidha wanyang'anywe simu kama hawaweza fata masharti au watolewe nje ya darasa waka ongee vizuri huko nje kama simu ina umuhimu kuliko kipindi.

Maadili Mashuleni (Kazi safi ya Haki Elimu)


Ni wazi kwamba serikali haiwezi kufanya kila kitu kudhibiti maadili ya wanafunzi ila inawezekana kwa ushirikiano wa wazazi, walimu ama walezi.Kwa wazazi kama unamnunulia mtoto wako simu ni vema umwambie matumizi ya hio simu akiwa shule, kwa walimu ni vema kuwaambia au kuweka tangazo linalo zuia matumizi ya simu muda wa masomo au darasani.Pia wazazi tuwe karibu na watoto wetu kujua hata wanaishi vipi na shule wanaendeleaje,utakuta mtoto ana simu ambayo hata baba au mama hawana (nina maana ya Gharama sana) mnunuzi hajulikani na simu hio hutumika wakati wa shule na usiku nyumbani wakati hata wazazi hio namba hawaijui.

Kama wazazi tunajiweka mbali na watoto wetu wa shule basi hata wasipo faulu tusilalamike.Ijulikane kwamba kusoma inahitaji moyo na faraja ya wazazi ni muhimu katika masomo.Ni lazima mzazi ujue maendeleo ya mwanao angalau kwa kila muhula.Kwakuto fatilia maendeleo ya mwanafunzi ndio siku ya siku unakuta mtoto wako ni mvuta bangi tu shule inamboa haitaki tena, kafukuzwa ana mimba (kwa wasichana) au tu amekua mtoto aliyekosa maadili kwa namna zote.Zamani mtu anaweza sema hajui sasa haki elimu ndio hao wanafichua maovu mashuleni.Wazazi,Waalimu pamoja na Serikali ni lazima tuwajibike sehemu zinazo tuhusu.

No comments: