Foleni kwa mbali ilikua kama hivi kuelekea Loliondo kwa Babu
4x4 ndio ulikua mpango mzima kuelekea kwa babu ukizingatia barabara zetu ni mbaya zaidi hasa mvua ikinyesha.
Huyu ndiye Babu Mwaisapile akiwa kazini na hatimaye kuiteka Bongo sasa hivi uki google Loliondo wonders utapata habari nyingi za huyu Babu kwenye vyombo vya habari ndani na nje ya Tanzania.
Babu anazidi kugawa 'dose'
Mheshimiwa na mpiganaji tegemeo naye alikuwepo...
Waheshimiwa pia walikuwepo...
Serikali haikua na namna bali kuunga mkono jitahada za babu pamoja na kuahidi kuwepo kwa 'research kuhusu dawa ya babu ambayo mpaka sasa HATUNA MAJIBU KAMILI ni matumaini baada ya utafiti huo kukamilika tutapata kueleweshwa..
Babu alipata mpinzani toka Mbeya na Kikombe cha Mbeya ndio hiki maandalizi yanaendelea
Huyu ndio Dogo wa Mbeya (17yrs) Kikombe chake kilikua bure
Kwa dogo Mbeya hali ilikua kama hivi..
Huyu mtoto sijui hata anajua hio ni dawa usikute anadhani CHAI!! kazi kweli kweli!
Kwa dada Tabora watu kibao kama kawa
Kikombe cha Moro kikiwa kina andaliwa..
Baadae Kikombe cha Moro mambo yakawa hivi.. na bei ni 200/=
Safari hii Kikombe ni Njombe kwa Dr Mwandulami (58) ni bure 'until further notice'
Wananchi wakipata Kikombe cha Dr Mwandulami Njombe Mkoani Iringa.
Sasa hapa tumwamini nani katika hivi vikombe?? Na je ni lini serikali itatuambia ukweli kuhusu hivi vikombe? Je ikigundulika vikombe ni 'fake' nani wa kulaumiwa/kuwajibishwa?.Kusema kweli huu mwaka ni waajabu na mwamko kama mlivyoona ni mkubwa watu wana amini vikombe sana.Tujiulize ni kwanini?? je ni kutokana na matatizo yetu kiafya au wewe unaonaje?.Wizara ya afya ituambie baada ya utafiti kukamilika ili wananchi wajue kama kweli tiba ipo au ndio propaganda tu.
No comments:
Post a Comment