22 March, 2011

NAMNA YA KUFELI SHULE KWA MAKUSUDI                                                            ??????


1.Usiwe na ratiba ya kujisomea

2.Usiende maktaba kusoma wala kujikumbusha ulivyo soma darasani kwa muda wako wa ziada.

3.Usisome vitabu, wewe soma tu 'summary' za notes na kamusi ili ujue tu maneno magumu ya kuwatishia wengine kua msomi na lugha ina panda kwa sana.

4.Susia vipindi ukijisikia uvivu lala tu wakati wenzio wako darasani au safiri safari ya mbali kula starehe huko

5.Kesha sana kila siku lala saa tisa usiku au kumi kabisa alfajiri wakati shule unatakiwa kuamka saa moja asubuhi kila siku.

6.Nenda club mara nyingi iwezekanavyo kama vipi kila siku ukiweza.
7.Kuwa mlevi na mwingi wa wanaume/wanawake wakati uko masomoni.

8.Wakati mwalimu anafundisha wewe piga story na rafiki yako na kubadirishana vi memo chini chini vya kuchekesha au cheza game kwe simu au chochote chenye game.

9.Ukipewa mtihani anza kufanya bila kusoma maelekezo kwanza.

10.Kua mtovu wa nidhani na unaye taka ugomvi kila siku na uende darasani ukiwa umelewa.

11.Usisome wakati unategemea kufaulu mtihani kwa miujiza.

12.Usisikilize walimu wako au walezi/wazazi wako.

13.Uwe mchelewaji kwenda  kwenye vipindi shule na uwahi kuondoka kwenda nyumbani/bwenini

14.Uwe mpenda sifa,mjuaji wa kila kitu, majivuno ya kwenu mna pesa shule sio ishu.

15.Mwalimu anapo fundisha usichukue notes kaa tu muangalie kama kideo na ongezea kusinzia ikibidi.

16.Usijali nafasi unayoshika baada ya mitihani yako 'after all is just a number!!

17.Waambie wenzio 'wametumwa na kijiji kuja kusoma ndio maana wanajituma sana' na wewe kusoma kwako sio ishu sana, after all shule ikishindikana unaweza kuwa konda wa magari ya''baba/mama,mjomba,shangazi, baba mdogo nk''

18.Ukipewa maswali ya kujibu usifanye yaangalie tu na hisabati soma kama notes usi kokotoe hata moja 'after all ni ugonjwa wa taifa' na kama mmepewa kazi ya kundi wewe usishiriki chochote endelea na mambo yako upate 'marks' za bure

19.Wakatishe wenzio tamaa ''kufauru darasani sio kufauru maisha'; ' wasomi mbona wengi halafu wote choka mbaya tu (kusoma sio dili)

20.Ukiwa hujaelewa darasani usiulize kisa utaonekana mjinga!

NB.Yaliyo tajwa baadhi  hapa juu kama yataepukika lazima ufauru shule (i.e kuanzia msingi mpaka vyuoni), hata hivyo sio lazima haya tu yakufelishe yako mengi zaidi yanayoweza fanya mtu afeli shule na pia si kila mtu anafeli akifanya haya kwani kuna sababu mbalimbali zenye athari tofauti baina ya mtu na mtu.

Je una la ziada? Nitafurahi kusikia kama kuna mengine ambayo yana mfelisha mwanafunzi akiwa shule/college/chuo.

No comments: