Mbali na hivyo vitendea kazi walivyo navyo mfano magari ni dalili tosha kwamba serikali yao iko makini katika ulinzi na usalama kwani magari wanayo ya uhakika mfano BMW X5, D529, Range Rover, Hummer,lambourgini, Lotus, Lexus,Jaguar,Ford,Astra, Landrover Deffender, Mecerdes Benz na nyingine nyingi bila kusahau helicopter ambazo zina nembo ya polisi na nyingine hazina ukitaka kuona picha zaidi ingia hapa http://www.google.co.uk/images?hl=en&source=imghp&biw=1276&bih=605&q=police+cars+UK&gbv=2&aq=f&aqi=g1&aql=&oq=&gs_rfai=
Pia kujua kama gari lako lipo barabarani kimakosa mfano kutokua na insurance, gari la wizi n.k sio lazima polisi akusimamishe akiwa kwenye gari lake either mbele au nyuma yako basi anaweza jua gari lako lina makosa na ukasimamishwa kwa mahojiano zaidi.
(camera ya kudhibiti mwendo na uhalifu barabarani-UK )
Aidha polisi ni washikaji/rafiki wa kila mtu na hawaogopwi kama wetu huko Africa, hawa wa huku UK unaweza hata ukaomba hata lift hawana noma provided makaratasi yako yapo valid maana unaweza kua kama panya alie ingia zizi la paka bila kujali litakalo tokea. Pia ukienda club wanakuwepo wengi tu nje pamoja na Ambulance tayari kuwabeba walio zidiwa na pombe (hahaha).Zaidi ya hayo wapo askari wa doria ambao wanazunguka mtaani kwa magari na baiskeli, pia kwa miguu.Changamoto yetu hapa ni serikali zetu kua makini na vitendea kazi vya maafisa wetu wa kulinda usalama mahali popote nchini
(Gari la polisi aina ya Range Rover)
No comments:
Post a Comment