30 June, 2010

Sikiliza Antvirus ya Sugu A.K.A Mr II

Hi ndio antvirus ya MR Sugu ambaye siku za karibuni aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa mahojiano kwa kilicho daiwa 'kutaka kuua kwa maneno'' kama vyombo mbalimbali vilivyo ripoti. Hata hivyo bwana Sugu amedai kuachiwa kwa kujidhamini yeye mwenyewe.Pamoja na mambo mengine watu wengi wanasema kukamatwa kwake ni kutokana na kua mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kwani kuua kisanii ama kimuziki ni neno la kawaida mfano: jamaa kaua leo stejini/jamaa kavunja mbaya... yaani kaimba vizuri zaidi au sasa nakuchana live ikiwa na maana 'sasa nakusema hadharani'

Hata hivyo hakuna anaye jua ukweli halisi ulioko nyuma ya pazia katika zogo hilo japo kua watu wame chanwa live katika huu wimbo maarufu kwa jina la antvirus.Binafsi pamoja na kuheshimu haki za binadamu (freedom of expression/freedom of speech) naona nyimbo iligusa zaidi maisha binafsi ya watu kwa mtindo wa kukashifu na sio kutoa ujumbe unao kemea uonevu ama ukandamizaji wa baadhi ya vituo vya Radio kwenye tasnia ya muziki maarufu kama bongo flava/hip hop.Ni mtazamo tu zaidi sikiliza wimbo then toa maoni yako kama jamaa yuko sawa au(sio sawa) na harakati za kuikomboa tasnia hio inayo daiwa kujaa unyonyaji wa hali ya juu,upendeleo na udididmizi wa chini chini.

No comments: