Kutokana na kwamba mada ilopita ilikua inahusu maana ya HATER sitatoa tena maana ya neno hilo hapa.Nimekua nikipitia vyanzo vya habari mbali mbali kuhusiana na ma-celebrity wetu ( watanzania), raia wa kawaida hata viongozi pia nje na ndani ya Tanzania. Nimekua nashindwa kupata maana halisi ya HATER hasa pale mtu akisema ukweli ama kinyume kuhusu mtu mwingine ambaye kafanya kitu kwa maendeleo yake binafsi. Pamoja na hayo kuna watu wanawasema watu wengine bila kua na chanzo sahihi ama ukweli wa jambo wanalo ongelea sasa sijui hawa wanaingia kundi gani?.
Mimi kuna siku nimekutana na mtu (jina kapuni) akimuongelea celebrity mmoja wakibongo (Mwana Falsafa ama Mwana FA) eti yuko HARVARD UNIVERSITY (USA) anasoma huko masters. Nikamuuliza kama habari kapata wapi akajibu mie huyo celebrity ni rafiki yangu kaniambia mwenyewe!!! Nikamuuliza anasoma nini huko Harvard? Akajibu sijui ila ni masters degree. Nikamwambia mie huyo celeb.. unaye msema nipo naye Chuo kimoja UK ila tuko kozi tofauti na pia anaishi mji mmoja na mimi. Kabla sijamalizia kuongea nikaitwa labda kama mimi ni HATER ila jamaa anasoma states. Sasa ndio nashindwa kuelewa maana ya HATER ni ipi yaani ni Yule anayesema ukweli ama anaye danganya ama msingizia mtu???!! Na kwanini mtu ukomalie kitu usichojua ukweli halisi??
Ok! Kama nilivyosema katika pita pita vyombo mbali mbali vya habari mtandaoni nikakutana na mtandao wa ma-celebrity mtu yule yule kasemwa kwamba yuko UK anasoma masters. Wakati huo huo kuna watu wakasema ni uwongo UK hasomi kwa sababu kozi anayodhaniwa kuisoma haipo katika hicho chuo. Kama haitoshi wakaendelea kudai kwamba kasoma na kumaliza kwa certificate level pale IFM. Pamoja na kwamba haiwahusu ila wamefatiliana kupata taarifa isiyo sahihi na kwa vigezo wanavyo vijua wao wakalalama kapata CERTIFICATE tu how comes asome Masters?? Kutokana na mjadala huo mkali waungwana wakasema sio CERTIFICATE bali ni Adavanced Diploma ndio maana kapata nafasi ya kusoma COVENTRY UNIVERSITY hapa UK.
Sasa sijui hawa ambao hawakua na habari sahihi kuhusu Mwana FA tuwaitaje? Maana sina hakika kama hawakutaka jamaa asome ama vipi? ivi kwanini mtu uongee vitu kwa msisitizo wakati huna FACTS? Na asingesoma wangefurahi ama kununa na inawahusu nini? Na zaidi ya hapo wanadai kama kasoma basi wanataka ona japo picha za mahafali dahh!!. Sina hakika hata kama wanajua mahafali ni lini? Pamoja na hayo mtu kumaliza chuo sio kufikia mahafali kwa sababu mbali mbali mfano:kushindwa kuhudhuria siku ya tukio,matokeo yasio ridhisha (Failed Report/dissertation), kuto maliza kulipa ada na mengine.
ANGALIZO…. Sina maana moja ya haya yana mhusu muhusika…!!! Sasa sijui kama wasipo ona hizo picha atakua hajasoma ama ni vipi duh!! wali mwengu bana!!
Hali kadharika neno HATER limekua maarufu kwa raia tu na hata viongozi. Mtu akifanya jambo la mafanikio katika maisha yake waosha vinywa hua hawakosi jambo liwe la kujenga ama kubomoa.Mfano: kuna watu kadhaa, nitatoa mfano mmoja, mtu mmoja katika kijiji chetu ambako miaka ya mwishoni mwaka 1980 nyumba za bati zilikua za kuhesabu. Sasa huyo jamaa alikua anataka jenga nyumba ya bati alichofanya ni kujenga mpaka akamaliza ndipo akaenda kununua bati bila hata kuchukua vipimo vya nyumba yake kwa madai WANAOTENGENEZA BATI WANAJUA SIZE YA NYUMBA ZOTE IKIWEMO YAKE KWAKUA YEYE NI FUNDI KUJENGA KWAHIO HANA HAJA KUPIMA JAPO ALISHAURIWA AKABISHA NA KUTAKA KUPIGANA NA KUSEMA ‘’HATERS WANANIZONGA KISA NAJENGA NYUMBA YA BATI’’….Mbaya zaidi mambo ya shop with confidence maarufu kama mali iliyo nunuliwa yaweza rudishwa hayakuwepo ama hayapo tofauti na huku UK ambako mtu una shop with full confidence!! wakati huo huo sisi mambo haya Africa ni nadra sana sana ipo MALI ILIYO NUNULIWA HAIRUDISHWI!!
Sasa kwa huyu jamaa na umbali wa sehemu duka lilipo pamoja na gharama za usafiri ilikua ni karibia nusu ya gharama ya bati zote bila kusahau MALI ILIYONUNULIWA HAIRUDISHWI kwa maana hio alishanunua mbuzi kwenye gunia ni zake hana kwakuzipeleka!. Ikafika siku ya kuezeka kuweka bati hazitoshi ni fupi akitaka zitoshe basi apige paa iliyo flat juu na ndivyo alifanya na kuhamia kabisa katika hiyo nyumba kwa shangwe na mbwe zote eti mvua imkome hanyeshewi tena hehehhe!! in 3 weeks time zile bati ziliondolewa na upepo na kubomoa sehemu kubwa ya nyumba! Wale walioambiwa HATERS ndio ilikua kimbilio…sasa mimi bado sielewi maana halisi ya HATER ni nini, je ni yule anayesema ukweli ama mwongo???? Mnisaidie maana ya HATER please!!
Tukija kwa upande wa siasa na uongozi kila mara twasikia Fulani kala rushwa mtu akiinua mdomo kusema basi ni HATER maarufu kama ‘’MTU MWENYE CHUKI BINAFSI AMA ZA KISIASA’’ Hii ipo pia kwa watu wa kawaida mfano mtu ununue gari basi ukipita mtu utaambiwa unaringa na kama haitoshi inaweza jengwa nyumba barabara unayopita ili ukose kwa kupita na gari lako sasa sijui hapa ni HATER ni yupi?
AU unakuta mtu kanunua mziki mkubwa kama ule wa club kaweka ndani halafu anapiga sauti ya juu tena usiku watu wamelala akiambiwa apunguze anasema HATERS wameanza majungu wanaona wivu sasa wanataka nikasikilizie wapi mziki wangu kwani na wao si wakanunue? Sasa hapa HATER ni yupi kati anaye nyima usingizi watu na anaye sema punguza sauti? Msanii akiambiwa track yake mbovu atasema aliyesema hivo ni HATER tena hawa ndo kabisa wanapenda kusifiwa tu sio kupondwa ama kukosolewa, japo wapo wanaoponda kwa maana ya kua HATER lakini wapo ambao wanakosoa kwa maana yakutaka mtu ajirekebishe Ivi HATER ni nani?......visa vya ma-HATER ni vingi hata wewe msomaji wangu wavijua waweza endeleza kuandika tujumuike wote hapa ila twambie HATER ni nani ok? hehehehe!
Well, nijuavyo mimi ni kweli jamaa kasoma COVENTRY UNIVERSITY kuanzia mwanzoni mwa 2009 na kumaliza mwanzoni mwa mwaka 2010. Na ratiba ya mahafali iko hivi kwa wenye kozi ya mwaka mmoja ( Masters): wale walioanza masomo mwanzoni mwa mwaka watamaliza mwanzoni mwa mwaka kwa mwana unaofata mfano: January na February Mahafali ni July, hali kadharika walio anza September intake wanamaliza September mwaka ujao na mahafali yao ni November ya mwaka huo Mfano:kuanza September 2009, kumaliza September 2010 na mahafali November 2010 yaani miezi miwili baada ya kukusanya dissertation yako ama kumaliza chuo kwa maana ya kumaliza kazi za chuo zinazo kamilisha degree yako.
Pamoja na mambo mengine, COVENTRY UNIVERSITY ni moja wapo ya vyuo vya bei rahisi ukilinganisha na vyuo vingine hapa UK pande za WEST MIDLANDS. Na kimekua kikipata umaarufu mwaka hadi mwaka kutokana na kuchukua wanafunzi wengi toka Africa wakiongozwa na Africa magharibi, Africa mashariki ikifuata, Africa kusini, Africa ya kati na kaskazini zikimalizia na hii yote ni kutokana na urahisi wa ada,maisha na usalama katika hili jiji la COVENTRY. Na kwa wale wenzetu wanaojua UK ni London basi si haba Coventry University wana Branch huko pia japo sina hakika kama ADA kwa London itakua sawa na ya Coventry ambayo ndio main campus.
Wakusoma karibuni ulaya ila uwe na moyo wa kipiganaji usiunge tu tela eti ''Naenda ulaya''!!!!huo ndo ukweli wa mambo, nikipata muda nitaleta''maisha halisi ya ulaya'' kaa mkao wa kula. Kwa leo naishia hapa, much love to you all by rijaki
No comments:
Post a Comment