28 April, 2012

MATANGAZO YALIYOSHAMIRI MAGAZETINI NA KWENYE MABANGO MITAANI


                                            Eti mafanikio siku 3, hivi hii imekaaje?

19 April, 2012

MZEE WA VIJISENTI WA NIGERIA AFUNGWA MIAKA 13

Gavana wa zamani wa moja ya majimbo tajiri Nigeria, (Delta State) bwana James Ibori afungwa miaka 13 jela.Bwana Ibori alikamatwa mwaka 2010 Dubai kwa makosa ya kujipatia mamilioni kwa njia ya udanganyifu.Mheshimiwa huyo wa ugavana jimbo tajwa kwa miaka ya 1997-2007 baada ya kukamatwa alipelekwa nchini Uingereza ambako alikua ameweka baadhi ya pesa na kununua majumba ya kifahari kwa mahojiano zaidi na polisi mpaka kufikia uamuzi huo wa kufungwa miaka 13 baada ya kuthibitika.Sambamba na hilo mheshimiwa atafilisiwa kwa maslahi ya taifa hilo kubwa kabisa balani Afrika,hususani Afrika Magharibi.


Jeshi la polisi nchini Uingereza lilishangazwa na manunuzi ya gavana ambaye inasemekana mshahara wake ni 4000£= 10Million za  Ki Tanzania kununua nyumba moja kwa gharama ya 2.2 million pounds sawa ma takribani Billion 2 na nusu za kitanzania, pia alinunua nyumba nyingine kwa  £ 311,000 (UK), pia kanunua mansion South Africa kwa £3.2Million, Magari kadhaa aina ya Range Rovers kwa £600,000, Gari aina ya Bentley £120,000, Mercedes Maybach kwa Euro 407,000.


Kweli Africa raha huyu ni kiongozi mmoja tu!! Je serikali zetu zina pesa kiasi gani? (TAFAKARI......!!!!!)


Kwa habari zaidi soma HAPA

10 April, 2012

KUMBE POLISI NAO HUIBIWA!!!

Habari toka majuu (Kwa Malikia/UK aka Ukerewe) zinasema maelfu ya pauni za Uingereza aka Great Britain Pound (GBP) yaliyokua mikononi mwa polisi yaibiwa. Pesa hizo ni zile ambazo zilikamatwa kutokana na upatikanaji wake kuhusisha njia ya udanganyifu na kuhifadhiwa katika ghala yenye ulinzi mkali katika kituo kimoja cha polisi wakati uchunguzi zaidi ukiendelea. Watu watatu walitiwa hatiani kuhusishwa na sakata hilo.Hata hivyo pesa hizo kiasi cha 113,000£ zapotea katika mazingira ya kutatanisha.Uchunguzi unaendelea na hakuna polisi wala raia aliyetiwa hatiani kutokana na upotevu huo..Inashangaza eti pesa ikaibiwa kituo cha polisi!!.Hivi polisi hazina bank accounts?.Kweli Duniani kuna mambo!!

Kwa habari zaidi soma HAPA

MAZISHI YA KANUMBA KUFANYIKA LEO KINONDONI MAKABURINI BAADA YA MISA NA KUAGWA RASMI VIWANJA VYA LEADERS CLUB




RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Kamati ya mazishi ya msanii Steven Charles Kanumba yatoa taarifa ya ratiba kwa vyombo vya habari ya utaratibu wa kumpeleka katika nyumba ya milele msanii huyo ambaye alikufa Ijumaa Aprili saba usiku.

Msanii huyo ambaye atazikwa katika makaburi ya Kinondoni amefanyiwa utaratibu ambao utamwezesha kila mwenye kuhitaji kushiriki mazishi hayo kuweza kumuaga. 

   Mwili wa marehemu utachukuliwa kwa msafara kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili saa 2.30 asubuhi. Utapitishwa barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi viwanja vya Leaders Club, Kinondoni ambako Misa ya kumuombea itasomwa pamoja na salamu mbalimbali kabla ya watu wote kumuaga. 

Kamati hiyo imetoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kuanzia saa mbili asubuhi kumuaga katika barabara ambazo atapitishwa . Saa 3.30 asubuhi mwili wa Kanumba utapokelewa viwanja vya Leaders ukitanguliwa na mapokezi ya wazazi wake, viongozi mbalimbali wa serikali ambao juu yao kabisa atakuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal. 

 Saa 4.00 itakuwa ni muda wa kusoma Misa ambayo inakadiriwa kuchukua dakika 60 na saa 5 itakuwa kipindi cha salamu kutoka kwa watu mbalimbali. Saa 6.00 mchana ratriba ya kumuaga Kanumba itaanza mpaka saa 9.00 alasiri na baada ya hapo utakuwa wakati wa kuusafirisha mwili kwa msafara kutoka Leaders Club mpaka makaburi ya Kinondoni.Msafara huo utapitia barabara ya Tunisia, utakatisha barabara ya Kinondoni kuelekea makaburini. 

Sa 10.00 maziko yatafanyika kwa kufuata taratibu za imani ya marehemu. Kamati hiyo ya mazishi inayoongozwa na Gabriel Mtitu imewaomba wananchi watakohudhuria shughuli hiyo kwenda na maua ili kumuaga kwa heshima. Ibada na maziko vitafanyika kadri ya imani ya marehemu. Utulivu, unyenyekevu na ustahimilivu ni mambo muhimu yanayohitajika katika kipindi chote cha kumuaga mpendwa wetu Kanumba. 

BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. Sisi wote tulimpenda kwa dhati na tulitamani aendelee kuwa nasi siku zote ila Mungu aliyemleta kwa mapenzi yake ameamua kumchukua. Jina lake lihimidiwe. 

                     K.N.Y GABRIEL MTITU MWENYEKITI WA KAMATI YA MAZISHI