20 June, 2011

MHESHIMIWA AMESEMA.....Mh Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini CHADEMA afunguka na Fiesta kama ifuatavyo.''Mbeya hatuhitaji upuuzi unaoitwa FIESTA,kwahiyo isije na naapa...uamuzi huu ni sehemu ya mapambano yetu dhidi ya maadui hawa wa maendeleo ya sanaa,and we are very serious on this one!!! Ujmbe huu umepatikana kwenye ukurasa wa muheshimiwa huko Facebook au kitabu cha uso.


Katika kuthibitisha kua hajiwakilishi mwenyewe au kutumia nafasi yake kuzuia fiesta Mbeya muheshimiwa Sugu ameongeza nanukuu ''HATUHITAJI FIESTA MBEYA,MI NAWAKILISHA TU MATAKWA YA VIJANA WA MBEYA...HASA WA MWANJELWA(SIDO) NDO WAMELILETA HILI KWANGU NA NINA FURAHA KUWA NAO NA KUHAKIKISHA MATAKWA YAO YANAKUWA...BY ANY MEANS NECESSRY'' mwisho wa nukuu.


Kibaraza hiki kina imani kwamba ujumbe huu una mengi yaliyojificha nyuma ya pazia na pengine watanzania wangependa kujua hayo yaliyojificha kabla ya kutoa maoni yao.Ukiangalia kwenye ukurasa wenye huo ujumbe (Facebook) maoni ni mengi na yenye mitazamo tofauti.Ni vema na haki muheshimiwa kuwakilisha watu wake lakini pia kuonyesha hao maadui wa sanaa ni wapi na uadui wao ukoje vinginevyo  kila mtu ATASEMA MHESHIMIWA ANATUMIA MABAVU KWA MWAVULI WA CHEO CHAKE KULIPIZA VISASI AU KUTOA KERO ZAKE BINAFSI huo ndio mtazamo wa kibaraza hiki kwani unaposema hili lifanyike/ lisifanyike ni bora kusema kwanini.


K wa habari zaidi:


No comments: