28 April, 2011

MALAWI WAMWAGA UGALI,UINGEREZA WAMWAGA MBOGA!!!

Ni katika sakata la uongozi unaodaiwa kuwa ni mbovu nchini Malawi ambapo aliye kua boss wa Malawi enzi za ukoloni ikiitwa Nyasaland (Uingereza/UK) ambaye pia ndio mtoa misaada mkuu nchini humo amesiitisha misaada hio tangu mwaka jana kwa kiasi cha Pauni Million 3 kutokana na matumizi mabovu ya serikali ya Malawi.Kwa mujibu wa gazeti la 'The Telegraph' matumizi mabovu ni pamoja na ununuzi wa ndege ya Rais Bingu Wa Mutharika kwa kiasi cha pauni million 8 kwa nchi masikini kama Malawi.

Katika sakata hilo Balozi wa Uingereza nchini Malawi  Mr Fergus Cochrane-Dyet ameamriwa kuondoka nchini humo kwa kosa la kuikosoa Serikali ya Malawi kwa matumizi mabovu na kunyima uhuru wa wananchi kuongea ama kuikosoa serikali kama ilivyo ripotiwa na wana harakati wa haki za binadamu.Kufuatia uamuzi huo wa Malawi, Uingereza nao wamemtaka kaimu balozi wa Malawi nchini Uingereza kuondoka mara moja. Amri hiyo imetolewa jana na  katibu wa Uingereza mambo ya nje William Hague

No comments: