31 March, 2011

MWAKA WA VIKOMBE NI HUU, MORO KUMEKUCHA KIKOMBE KINGINE!!

Baada ya Babu wa Loliondo kuvuma kwa kasi ya ajabu tukasikia wa Rombo (fundi baiskeli) bahati mbaya hakuvuma!!!,kaja dogo wa Mbeya Mabatini, mara dada wa Tabora wote bei ya KIKOMBE ILIKUA Tshs 500/= na sasa ni Dada wa Morogoro!!. Tena huyu kaja na 'sale' KIKOMBE 200/=. Toka tusikie KIKOMBE  watu Kibao wapo bize na Vikombe sasa mie sijui  ngoja tuone mwisho itakuwaje HUU MWAKA WA VIKOMBE, inatishaa..


Kwa habari zaidi tembelea kero nyingi blog hapa: http://keronyingi.blogspot.com/2011/03/breaking-news-kuna-dada-wa-mji-kasoro.html

2 comments:

H. J. Simaya said...

Dah... inanibidi nianzishe changu...bei ya promotion sh 100.

Rik Kilasi said...

hahahhaha haya bana mie ntakua muhasibu wa babu Hassan.Toa taarifa rasmi kabisa ili niandike hapa KIKOMBE KINGINE CHAIBUKA COVENTRY lol.

Ila hii hali inatisha kusema kweli mie sielewi hivi VIKOMBE mwisho wake utakuwaje au ndio yale yale matatizo yetu kwa wengine ni mtaji au dili?