01 March, 2011

Gaddafi azidi kuishangaa dunia..

Kanali Gaddafi anazidi kuishangaa dunia kwa kumshinikiza ajiuzulu eti wananchi wamemchoka.Gaddafi anauliza ajiuzulu kutoka wapi wakati yeye sio Mfalme wala Rais na pia watu wake wanampenda kiasi cha hata kufa kwaajili yake?.Amesema hayo alipo hojiwa na BBC huko Libya.Ameongeza kuwa wanao andamana ni Al-Qaeda na watu walio wengi ni mashabiki wake na si vinginevyo.Amemalizia kusema Dunia haiijui Libya ni nini na ina serikali ya namna gani ndio maana wana muharibia.''Libya watu wangu wananipenda, hao wengine ni Al-Qaeda'' Gaddafi alisema.
(BBC)
Zaidi soma hapa:http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-12603259

No comments: