Aliyekua Rais wa Misri (Egypt) bwana Hosni Mubaraka aachia ngazi baada ya mgomo wa kudai aachie madaraka kudumu kwa siku 18.Mubaraka amekua akitoa ahadi mbali mbali kuwapooza wananchi ambao wamemchoka wakimtaka aondoke madarakani mara moja ndipo wakae kuzungumza mustakabari wa nchi hiyo ya Misri.Ahadi hizo ni pamoja na kusema mtoto wake ama yeye mwenyewe hawata gombea muhula ujao.Wakati huo huo aliweza kumteua makamu wake mpya ambaye wanachi waliweza msikiliza japo kidogo.
Zoezi hilo lilionekana kushindikana kwani mgomo uliendelea kama kawaida hata baada ya kutangaza kua amempunguzia makamu huyo baadhi ya madaraka yake.Pia aliahidi kuachia ngazi ila wampe muda na sio kumuondoa ghafla kitu ambacho kingeleta machafuko inchini humo.Wakati huohuo Uingereza na Marekani zilipinga hio kali kwa kusema wananchi ndio walio amua, hakuna nchi itamlazimisha ajiuzulu ila asikilize kile wanachi wanataka.
Kabla ya giza kuingia inchini Misri siku ya tar 11/02/2011 vyombo vya habari ikiwemo BBC vilitangaza kutoweka kwake mjini Cairo ambako ndio makao makuu ya nchi hio na kuelekea sharm-el sheikh (Mwambao mwa bahari Nyekundu -Misri) kwa mapumziko baada ya uongozi wake kudhoofu kiasi cha kwamba jeshi la nchi hio lime mshauri aachie ngazi.
Rais huyo aliyeshikilia madaraka kwa miongo takribani mitatu mfululizo tena bila dalili ya kuachia ngazi pamoja na kwamba ni mzee anaye hitaji kupumzika, amelazimika kuachia ngazi kwa shinikizo kubwa la wanachi wake walio jaa nje ya Ikulu wakimtaka ajiuzulu kwani wamemchoka.Misri kwa sasa ipo chini ya jeshi la nchi hio mpaka uchaguzi utakapo fanyika mapema mwaka huu.
No comments:
Post a Comment