16 February, 2011

Mabomu yalipuka Gongo la mboto jijini Dar

Imeripotiwa kutokea mlipuko wa mabomu jijini Dar es salaam eneo la Gongo la mboto.Watu kadhaa walisambaa eneo hilo wakikimbia huku na kule kunusuru maisha yao.Hata hivyo bado haijajulikana chanzo cha mlipuko huo na hata maafa yaliyotokea.Hali kama hii imewahi tokea mwaka 2009 Mbagala ambako ghala la mabomu lilipuka na kusababisha uharibifu mbali mbali katika eneo hilo.Stay tuned Kwa habari zaidi nini chanzo cha mlipuko huo na hata madhara yaliyotokea.

Moja ya taswira ya mlipuko wa mabomu kwa mbali:


Taarifa ya polisi katika video kupitia ITV.Too many questions to ask watu watatuliaje mbele ya bomu? Ye mwenyewe asingeweza kutulia hapo ITV akisikia kuna bomu
Anyway msikilize mheshimiwa akitoa taarifa

2 comments:

Anonymous said...

Rais Kikwete tuna mlaumu bure utendaji mbovu wa utawala wake mtu muhimu kama huyu hawezi kutokua siriaz kiasi hiki, kwanza ameongea pumba, pili ana swing kwenye kiti''dalili ya starehe kukolea,tatu si kazi yake kwa muda ule kutoa ile taarifa ambayo ni utumbo mtupu.Narudia kusema Kikwete ana machache ya kulaumiwa kwa utawala mbovu ikiwa ni pamoja na kuchagua wasaidizi ambao hawana uwezo kushika nyadhifa walizopewa.
Huyu anaye yumbayumba akiwa ni moja ya watu ambao sina hakika kama anajua hata kazi yake.

Rik Kilasi said...

Umeona eeh habari ndio hio hata tuwe na Rais malaika kama wasaidizi,washauri,wataalam n.k wakifanya ovyo basi hata onekana mchapa kazi tena.Kumbuka mkuu wa kitengo siku zote hubeba lawama pale mradi au kitengo chake kitapo enda ovyo kwahio sishangai kwa hili japo ni muhimu kujifunza mambo kama haya tena ya aibu yasirudie,wananchi tuna shida zetu na mabomu tulipuliwe haki iko wapi?

Well kuna mengi yamejificha utawala wa nchi nyingi za kiafrica ila tu ipo siku itajulikana kama viongozi hawajifunzi, watu siku hizi wanaelimika.