20 February, 2011

Mgomo Libya waongeza idadi ya vifo..


Muammar Abu Minyar al-Gaddafi (Rais wa Libya)

Idadi ya waliokufa kutokana na machafuko yaliyotokea Libya imefikia imeongezeka mpaka kufika 84.Libya ambayo ipo chini ya Rais Muammar Abu Minyar al-Gaddafi ambaye aliingia madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka 27.Imeingia matatani muda mfupi baada ya machafuko ya Egypt/Misri ambapo Rais wa nchi hio amejiuzulu February 11 kufuatia mgomo wa nchi nzima kwa takribani siku 18.Mubarak alifata nyayo za Rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali ambaye alijiuzulu January 2011

Libya imeripotiwa kutumia silaha nzito za kijeshi kukomesha mgomo unaozidi kuenea inchini humo.Pia wanahabari wakimataifa wamepigwa marufuku kuingia Libya kiasi cha kuwa vigumu kupata taarifa halisi ya kinacho jiri nchini humo.Facebook,Aljazeera na mitandao ya simu imesitishwa.Mpaka sasa jeshi la nchi hio lipo mtaani kudhibiti mgomo ambao unazidi kuongezeka kutokana na kinacho daiwa kunyimwa hata muda wa kuzika wenzao walikufa katika mgomo huo ambapo watu kadhaa wanadaiwa kuuwawa kwenye mazishi ya baadhi ya waandamanaji waliopigwa risasi hadi kufa

Zaidi soma:http://www.abc.net.au/news/stories/2011/02/20/3143581.htm?section=justin AU http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-12512536


Ramani ya Libya

Muammar Gaddafi Rais tangu 1969
Idadi ya watu Libya ni 6.5m
Wananchi wamesoma kwa asilimia 88
Muda wa mtu kuishi ni maika 74 wanaume na 78 wanawake.
Kipato cha raia kwa kichwa: $12,020 (World Bank 2009)

No comments: