03 July, 2010

Huyu ndiye aliyekua Loon.....

Wakati wasanii wetu wengi wa muziki wa kibongo wanachukua video kwenye nyumba,magari ama maeneo mazuri kwa ujumla hali iko tofauti kwa msanii Loon alipotembelea Bongo.Msanii huyo ameonekana katika Video yake kwa jina 'Distracted' akiwa bongo ambako mazingira aliyo chukulia video ni sambamba na hali halisi ya makazi ya walio wengi bongo/Tanzania.Zaidi angalia video hii hapa chini.

Hata hivyo msanii huyo ambaye sasa katoka kivingine kabisaaa kwa kuwaunga mkono Busta Rhyms,Napoleon,Akon,Ice Cube, na wengine wengi ambao wameukacha Ukisto na kua waislam.Kama Video ya pili inavyo onyesha hapa chini.

Si vibaya zote ni imani tu ili mradi kote wana amini Mungu yupo.Kwa upande mwingine mashabaki wanauliza kwa mtindo wa kutoa maoni hasa 'YOUTUBE' na kushangaa zile ndevu kama ndio kua na imani kali ama laa na wengine kushangaa mtu mweusi kuiga style za waarabu kwa kufuga ndevu kiasi kile kwani anatisha.Wakati huu Loon anasema yeye ni good boy na sio bad boy tena kama alivyokua under bad boy Records.Kazi kweli kweli.Loon wa sasa ndio huyu

3 comments:

Anonymous said...

Kama Hujui Dini ya kiislam usiropokee Uarabu, kwanini usiwaulize hao mashabiki, kwani yesu Mwafrika!!!? mbona anawafuasi waafrika.

Rijakis said...

Dah naona imeku touch, well n good!.Kwa faida ya wengine ningeomba utwambie ufugaji wa ndevu na dini ya Uisilamu ili tusitok nje ya mada.

NB: Naheshimu dini yoyote inayo heshimuna na kutambua uwepo wa Mungu!.Changia kutoa changamoto na si vingenevyo.Shukrani na karibu sana 'The Network'

Anonymous said...

Mbona Busta Rhyms,Akon na wengine hawaja fuga ndevu kama osama na ni Waislam wa kusilimu?.Tuelezeni ndevu zile ndefu zina maana gani katika Dini ya kiislam na kwanini wengine hawafugi zile ndefu na ni waislam coz hapa swala ni Loon anatutisha na midevu yake Lol!